Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 7 3
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Mifumo yetu binafsi ya kupokea na kuchuja maoni mara kwa mara inazuia uelewa wetu wa mazingira ya kihistoria ya maandiko.
4. Tumezoezwa kusoma maandiko kama tunavyoyasoma siku zote (yaani, tunaingiza tafsiri za usomaji wa zamani katika usomaji wetu wa sasa).
5. Tunaharakisha kutoa hitimisho bila kuzingatia andiko lilimaanisha nini kwa wasomaji au wasikilizaji wa kwanza.
C. Mtazamo muhimu unaohitajika: unyenyekevu , Yakobo 1:5
2
1. Kutambua muda mrefu unaotutenganisha na muktadha halisi wa andiko.
2. Utayari wa kukiri tofauti na vizuizi vilivyopo kati ya wakati wetu na ule wa waandishi na hadhira ya maandiko.
3. Utayari wa kuahirisha hitimisho hadi tutakapojifunza zaidi kuhusu muktadha asilia kabla ya kuhitimisha juu ya kile ambacho andiko lilimaanisha lilipoandikwa.
4. Kutunza kwa dhati heshima ya maana na muktadha asilia.
D. Hatua za kuelewa muktadha asilia.
1. Chukua muda kufanya yakupasayo ili kutafiti kuhusu muktadha asilia, Mit. 2:1-6.
2. Heshimu mchakato wa uchambuzi yakinifu, Ezra 7:10.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker