Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
8 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yametokana na video. Katika kipindi hiki tumeona jinsi Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu bora ya kutafsiri Biblia iliyotengenezwa ili kutusaidia kuelewa ukweli wa maandiko na kuziba pengo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa. Kama wanafunzi wa Neno, tunahitaji mbinu ya kutafsiri maandiko ambayo inaheshimu asili ya maandiko kama fasihi ya kale, pamoja na Roho Mtakatifu aliye hai katika Kanisa ambaye ni mwalimu na kiongozi wetu tunapotafuta nia na mapenzi ya Mungu (1Kor. 2:9-16). Pitia ulichojifunza katika video kupitia maswali yafuatayo, na utumie maandiko kujenga hoja katika majibu yako. 1. Nini maana ya Mbinu ya Hatua Tatu ya kutafsiri Biblia? Ni kwa namna gani mbinu hii imetengenezwa hasa ili kutusaidia kuziba pengo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa? Kwa nini tendo hili la kuziba pengo la umbali kati yetu na ulimwengu wa Biblia ni muhimu sana ili kuweza kutafsiri Biblia kwa usahihi? 2. Ni wapi katika Biblia ambapo maandiko yanaonyesha kwamba ili kuelewa maana ya andiko ni muhimu kuzingatia mbinu fulani ya kujifunza Neno la Mungu (taz. Mdo. 17:11; Isaya 8:20; Ezra 7:10; nk)? 3. Elezea faida na tahadhari zinazoambatana na matumizi ya mbinu yoyote katika kutafsiri Biblia. Ni mambo gani yanayoweza kutusaidia na kutulinda dhidi ya kutegemea sana mbinu na ufahamu wetu tunapotafuta kugundua kweli za Mungu katika maandiko na kuzitumia maishani mwetu? 4. Kwa nini sikuzote ni muhimu kukumbuka “picha kubwa” na “ujumbe mzima” wa Biblia tunapojifunza “vifungu” mahusi vya maandiko? Ni kwa njia gani somo lolote la Neno la Mungu kwa namna fulani linapaswa kuhusianishwa moja kwa moja na kufafanua ujumbe wa ufunuo wa mwisho wa Mungu kwetu kupitia nafsi na kazi ya Yesu Kristo? Tolea mifano jibu lako. 5. Eleza kwa ufupi mbinu ya sarufi ya kihistoria ya kujifunza Biblia na namna inavyohusiana na Mbinu ya Hatua Tatu . Kwa namna hiyo, ni jinsi gani Mbinu ya Hatua Tatu inatusaidia kuelewa maana iliyo wazi ya kifungu, na muunganiko wa ujumbe mzima wa Biblia? 6. Kwa nini ni muhimu kuheshimu umoja wa maandiko kama yalivyotujia katika aina zake mbalimbali (k.m., mashairi, nyimbo, nyaraka, historia, n.k.), na ni jinsi gani Mbinu ya Hatua Tatu hutusaidia kufanya hivyo? 7. Eleza kwa ufupi sababu muhimu zinazohusika katika kila hatua ya Mbinu ya Hatua Tatu . Ni kwa jinsi gani kila moja ya hatua hizo tatu inatusaidia kushinda baadhi ya matatizo yanayohusiana na kuelewa kile ambacho
Sehemu ya 1
Maswali kwa wanafunzi na majibu
page 321 3
Si tu kuijua, bali pia jinsi ya kuitumia
Paulo anapomwambia Timotheo ajitahidi kuwa mtu mwenye “kutumia kwa usahihi neno la kweli” ( 2 Tim. 2:15 ), maana yake ni kwamba kuna uwezekano hatari wa kutolishika Neno la Kweli na kutolitumia kwa usahihi. Na hilo linaibua maswali muhimu kuhusu namna ya kutafsiri Biblia. Ili kuiendea Biblia kwa hekima ni muhimu si tu kuijua, bali pia jinsi ya kuitumia. ~ Donald a. Carson. New Bible Commentary: 21st Century Edition . (Electronic Ed. Of The 4th Ed.). Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 1997.
2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker