Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 8 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Biblia inafundisha kama maandiko ya kale yaliyoandikwa katika lugha ambazo hazizungumzwi tena au kutumiwa kama zilivyokuwa wakati wa kuandikwa kwa Biblia? Elezea jibu lako vizuri. 8. Unyenyekevu, umakini, na kupenda uhuru katika Kristo huathirije uwezo wetu wa kulifahamu na kulitumia Neno la Mungu? Kuna uhusiano gani kati ya mtazamo na mbinu katika kutafuta kutambua maana ya Biblia? Kipi ni muhimu zaidi kati ya mtazamo na mbinu? Toa mfano ili kufafanua maoni yako. 9. Elezea na utetee kauli hii: “namna yoyote halali ya kutafsiri Biblia lazima ilenge kulifahamu Neno la Mungu kwa dhumuni la kuleta badiliko katika maisha, na si habari ya kujaza taarifa akilini.” Je, Mbinu ya Hatua Tatu inasaidiaje kuweka mkazo wetu katika badiliko la maisha na sio uchanganuzi wa maandiko na misamiati peke yake?
2
Hemenetiki ya Biblia: Mbinu ya Hatua Tatu Sehemu ya 2: Matumizi ya Mbinu ya Hatua Tatu : Kujifunza kutoka kwa Mtume Paulo
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Mbinu ya Hatua Tatu ya kutafsiri Biblia ni njia nzuri ya kutambua maana ya maandiko, na inaweza kuelezewa kivitendo kupitia mfano wa barua ya Paulo kwa Wakorintho, katika waraka wake wa kwanza, sura ya 9:1-14. Kwa kutumia mbinu hii katika kuchanganua kifungu hiki, tunaona jinsi gani kujifunza Biblia kwa nidhamu kunavyoweza kuleta matokeo makubwa na mazuri. Lengo letu katika sehemu hii, Matumizi ya Mbinu ya Hatua Tatu : Kujifunza kutoka kwa Mtume Paulo , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu bora ya kutafsiri Biblia ambayo inaweza kutumika vizuri katika kushughulika na migawanyo mbali mbali ya maandiko (maneno, aya, sura, vitabu, sehemu). Maagizo ya Paulo kwa Wakorintho katika 1 Wakorintho 9:1-4 yanatupa kielelezo cha wazi cha namna matumizi ya mbinu hii yanavyoweza kuleta manufaa makubwa. • Kila kujifunza Neno la Mungu huanza na kunyenyekea kwetu kwa Roho Mtakatifu, ambaye peke yake ndiye mwandishi wa maandiko na ndiye pekee anayetosha kutufundisha maana na umuhimu wa maandiko katika maisha yetu leo.
Muhtasari wa Sehemu ya 2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker