Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
8 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
• Hatua ya kwanza katika kutumia Mbinu ya Hatua Tatu ni kuchunguza kwa undani yaliyomo katika andiko, kubainisha usuli (historia) wa kitabu, mwandishi wake na hadhira, madhumuni ya kuandikwa kwake, pamoja na namna lilivyotafsiriwa katika tafsiri mbalimbali. • Kupata kanuni za jumla za andiko au kifungu ni hatua ya pili ya Mbinu ya Hatua Tatu , na inahusisha kutafuta jumbe kuu, kweli, maagizo, au mafundisho yaliyomo katika kifungu. Hatua hii inahusisha kuangazia maana ya kifungu katika mazingira (muktadha) yake ya asili , na hatimaye kile ambacho kifungu kinamaanisha kwetu katika maisha yetu leo . Kanuni hizi lazima zielezwe waziwazi, zikilinganishwa na mafundisho mengine ya Maandiko Matakatifu ndani ya Biblia, na kufafanuliwa zaidi kwa faida ya kujifunza kwa kina na kulitumia Neno la Mungu kwa ufanisi zaidi. • Baada ya kuona maelezo na kuchota kanuni zilizomo katika maandiko, tunaenda kwenye hatua ya tatu ya Mbinu ya Hatua Tatu ambayo ni lengo letu la kutendea kazi kanuni za kiroho katika nguvu za Roho Mtakatifu. Kutendea kazi Neno ni kitendo cha kuelekeza moyo kwenye Kweli ya Neno la Mungu kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu . Hili linahitaji uwezo wa kupambanua na utayari wa kutii mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. • Tafsiri yoyote ya Biblia imetolewa ili kuimarisha ufuasi wetu katika Kristo, na kimsingi ni njia ya kufafanua kwa namna tofauti tofauti mada zinazosisitizwa katika maandiko yote, lakini zenye ujumbe mmoja . Kiini cha maadili ya Biblia katika Agano la Kale na Jipya kinajumlishwa katika kumpenda Mungu na kumpenda jirani na kutumia uhuru wetu kuwajenga wengine na kumtukuza Mungu. Kwa sababuBiblia niNeno laMungu, ni muhimu sana kukuza unyenyekevu tunapoisoma, kukuza hali ya maombi na kutafakari tunapoitafakari na kujifunza, kutafuta msaada wa Roho Mtakatifu tunapojaribu kuielewa na kuitii, kuungama dhambi na kutafuta usafi wa moyo na nia na mahusiano tunapokua katika ufahamu. Kushindwa katika maeneo haya kunaweza kutengeneza wasomi, lakini si Wakristo waliokomaa. Zaidi ya yote, lazima tukumbuke kwamba siku moja tutatoa hesabu kwa Yeye aliyesema, “mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu” (Isa. 66:2). ~ Carson, Donald a. New Bible Commentary: 21st Century Edition . (Electronic Ed. Of The 4th Ed.). Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 1997. Unyenyekevu Ufunguo wa Kufasiri Maandiko
2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker