Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

9 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

4. Linamhusu kila mtu kila mahali (linaonyesha mapenzi ya Mungu au mawazo ya Mungu juu ya somo au mada fulani).

5. Linaweza kuelezewa kwa njia rahisi, iliyo wazi na inayoeleweka kwa wengine.

C. Jinsi ya kupata kanuni ya kibiblia.

1. Jifunze kifungu chako kwa kina, ukitazama maelezo na kupata maana zake katika “ulimwengu wao.”

2

2. Tafuta mafundisho au mawazo makuu yanayoelezewa katika kifungu.

3. Weka kanuni yako/zako katika kauli au tamko rahisi: wale walioitwa katika huduma wanaruhusiwa kujipatia riziki kupitia huduma hiyo.

4. Tamka katika maneno machache .

5. Iweke katika muundo wa kauli au mithali .

6. Tumia lugha iliyo wazi na rahisi kadri iwezekanavyo.

7. Hakikisha kuwa kauli yako:

a. Ni muhtasari wa yote uliyojifunza : usifanye kazi ya kina na makini katika hatua ya kwanza na kisha ukapuuzia matokeo ya kazi yako unapotengeneza kanuni.

b. Inaelezea maana ya kifungu cha maandiko ulichojifunza: inaeleza kiini cha ujumbe wa andiko husika.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker