Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 9 3
K U T A F S I R I B I B L I A
D. Ijaribu kanuni yako (yaani, mithali au kauli yako) kwa kuilinganisha na yale ambayo Biblia nzima inasema (1 Thes. 5:21).
1. Angalia NYUMA kwenye kifungu chenyewe. (“ Je, kifungu hiki kweli kinafundisha kile ninachodhani? ”) Jiulize kwa uaminifu, “Kama mtu mwingine angesoma kifungu hiki je, kuna uwezekano kwamba angeweza kugundua kanuni hii ambayo nimeigundua?”
2. Angalia KUPITIA vifungu vingine vya Biblia. (“ Je, kuna vifungu vingine katika Biblia vinavyoeleza wazi na kuunga mkono kanuni niliyoitengeneza? ”)
2
3. Angalia NJE ya kifungu uone mifano, simulizi, na vielelezo vya Biblia. (“ Je, maisha ya watu na matukio katika Biblia vinaendana na kanuni niliyoitengeneza? ”) Ikiwa huwezi kupata kauli au simulizi nyingine katika Biblia zinazounga mkono kanuni yako basi huenda katika eneo hilo hujapata kanuni ya kibiblia.
4. Angalia KATIKA vitabu vya ufafanuzi wa Biblia na mafundisho ya Kanisa ili kuona kama matokeo yako yanaungwa mkono na wasomi wengine. (“ Je, wengine wamepata maarifa sawa na haya ninayodai kuyapata hapa? ”)
a. Ikiwa hakuna mtu mwingine uliyemsoma ambaye amewahi kupata kanuni uliyoigundua, haimaanishi moja kwa moja kuwa umekosea, lakini hiyo ni ishara kwamba unahitaji kuwa mwangalifu sana.
b. Pasipo uungwaji mkono kutoka kwa wengine lazima uwe na utetezi wenye hoja makini sana za kibiblia na angalau ujaribu kueleza kwa nini wengine hawakuona kanuni hii.
5. Rekebisha kauli (kanuni) yako ili iendane na matokeo ya uchunguzi wako.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker