Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 0 9

K U T A F S I R I B I B L I A

1. Kwa lengo la kufanya mapitio, taja nyenzo za Biblia zinazochukuliwa kuwa “zana za msingi za ufasiri wa Biblia.” Na eleza kwa nini zana hizi ni za msingi sana katika kutupatia mtazamo wa kuaminika wa Neno, hasa sisi tuliokabidhiwa jukumu la kuongoza na kulisha wengine katika Kanisa. 2. Ni zana zipi za ziada tulizoziangazia katika sehemu hii ambazo zimeundwa ili kuongeza uwezo wetu wa kuziba pengo kati ya ulimwengu wa Biblia na ulimwengu wetu wenyewe. Kati ya zana hizi za ziada, ni ipi/zipi unaamini ni muhimu zaidi kuliko zingine, hasa kwa viongozi wa mijini katika wajibu wao wa kutunza roho za wanafunzi wa Kristo wa mijini? Elezea jibu lako. 3. Taja baadhi ya visaidizi vikuu vya rejea mtambuka muhimu kwa kazi ya ufafanuzi wa Biblia, na eleza ni nini hasa visaidizi kama hivyo hutuwezesha kufanya kuhusiana na vifungu vya maandiko. Je, visaidizi hivi husaidia kwa kiasi gani kukuza uelewa wetu wa maana ya kifungu au kitabu? Ni tahadhari gani zinazopaswa kuzingatiwa tunapovitumia katika kujifunza kwetu? 4. Ni vitabu gani mahususi vya rejea ambavyo vinajikita katika kutupa ufahamu wa historia, utamaduni, desturi za kijamii, watu, na mazingira ya kijiografia ya ulimwengu wa Biblia? Ni faida gani kuu tunazoweza kuzipata kwa kuunganisha zana hizi katika kujifunza maandiko? Ni mambo ya aina gani tunayopaswa kukumbuka tunapotafuta kufaidika na utafiti mzuri uliomo ndani yake? 5. Ni zana zipi za kibiblia ambazo ni muhimu hasa katika kutusaidia kupata taarifa za usuli kuhusu mwandishi, tarehe, na mazingira ya kitabu, na matumizi fulani maalum ya lugha katika Biblia (k.m., taashira, sitiari, lugha ya kitamathali, n.k. )? Ni aina gani za tahadhari tunazopaswa kuzingatia tunapotumia nyenzo hizi katika kujifunza? 6. Kwa nini vitabu vya ufafanuzi ni zana za kipekee za rejea, vikilinganishwa na zana zingine nyingi zilizotajwa hapo juu? Ni aina gani kuu nne za vitabu hivyo zinazopatikana kwetu leo, na kila aina hutumikaje hasa? 7. Ingawa vitabu vya ufafanuzi ni visaidizi muhimu sana katika kutoa ufahamu tunaohitaji na wa kina wa vifungu na vitabu vya Biblia, ni kwa namna gani havipaswi kamwe kutumiwa? Je, mfululizo wowote wa ufafanuzi, hata kama unafaa au ni mzuri sana, unaweza kuchukua nafasi ya jitihada zetu binafsi za kujifunza maandiko wenyewe? Elezea.

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker