Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 1 1

K U T A F S I R I B I B L I A

³ Biblia iliandikwa katika lugha tatu (Kiebrania, Kiaramu, na Kiyunani), na kwa sababu hiyo tunahitaji tafsiri nzuri ya maandiko katika lugha yetu ya asili. Tafsiri ni ngumu , hasa kwa sababu ya tofauti za lugha, tofauti za kitamaduni, umbali wa kihistoria, na mitazamo na falsafa tofauti kati ya watafsiri. ³ Konkodansi huorodheshamaneno yote ya Biblia namahali yanapopatikana kwa mpangilio wa alfabeti, na leksimu zinatoa ufafanuzi (matumizi) ya maneno kama yalivyotolewa katika mstari fulani wa maandiko. Kamusi za ufafanuzi huongeza maoni kuelezea uhusiano kati ya maana ya maneno na mafundisho ya kibiblia. ³ Kamusi za Biblia huorodhesha taarifa za kihistoria, kijiografia, kitamaduni, kisayansi, na kitheolojia kuhusu watu, mahali, wanyama, matukio, na vitu halisi vinavyopatikana katika Biblia, na pia muhtasari wa kila kitabu cha Biblia. ³ Vitabu vya mafafanuzi ya kieksejesia hutoa maoni ya kitaalamu kuhusu maana halisi ya maneno katika matini asilia, ikijumuisha masuala ya sarufi, maana za maneno, matokeo ya uhakiki wa Biblia, na taarifa za kihistoria na kiutamaduni ambayo yanaweza kuathiri ufasiri wa matini. ³ Bila kujali zana tunazotumia, tunapaswa kutumia nyenzo za rejea kwa wingi, lakini kila wakati tukikumbuka kwamba matumizi sahihi ya zana hizo ni yale yanayoweka wazi maana za maandiko, na sio kukataa au kupunguza umuhimu wake. ³ Zana za ziada ambazo tunapaswa kujifunza jinsi ya kuzitumia ni pamoja na tafsiri kadhaa tofauti za Biblia, atlasi ya Biblia na kitabu cha mwongozo wa Biblia, Biblia ya mada, kamusi ya theolojia, na vitabu vya ufafanuzi wa kitheolojia. ³ Visaidizi vya rejea mtambuka ( cross-references ) vinaangazia uhusiano wa matini na vifungu mbalimbali ambavyo vinazungumzia mada moja au vina kiini kimoja cha mada katika ufafanuzi wa Biblia (k.m., Biblia za mada, Biblia za rejea mtambuka, na miongozo ya mada na konkodansi). Ingawa haya yanatusaidia kuhusianisha maandiko katika somo fulani, ni lazima tuwe waangalifu tusifanye makosa ya muktadha tunapounganisha aya, na tukumbuke kila mara kwamba wahariri wanaweza kuhusianisha vifungu kwa namna isiyo halali na isiyoweza kutetewa. ³ Zana fulani hutoa usuli wa historia, utamaduni, desturi za kijamii, watu, na mazingira ya kimwili ya ulimwengu wa Biblia. Hizi ni pamoja na kamusi za Biblia, ensaiklopidia za Biblia, atlasi za Biblia na vitabu vya mwongozo,

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker