Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

2 1 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

MIFANO

Kutoka katika ukurasa hadi mimbarini

(Imetokana na hadithi ya kweli). Hivi majuzi katika kanisa moja lililokua la mjini, mchungaji mmoja aliondolewa cheo chake kama Mchungaji Kiongozi kwa sababu iligundulika kwamba kwa kiasi kikubwa alikuwa akisoma tu mahubiri yake kutoka katika kitabu, bila kuhariri, kunukuu, au kueleza kwamba alikuwa akifanya hivyo! Baraza la wazee lilihuzunishwa sana na jambo hili, kiasi kwamba waliona ni muhimu kusitisha huduma yake katika kanisa, si kwa sababu ya masuala ya kitaaluma bali kwa sababu ya masuala ya kiroho. Walihoji, inaleta picha gani kiongozi wa kiroho kukariri neno kwa neno mawazo ya mtu mwingine kama yake, huku ni kama hawezi kulipa kusanyiko na watu neno jipya zaidi, bora zaidi, na la uwazi zaidi alilolipokea kutoka kwa Bwana kwa ajili yao? Unafikiri nini kuhusu hali hii—kutegemea zana na nyenzo za wengine kumewafanya viongozi wengi wa Kikristo kuwa wavivu, wasioweza kutafakari upya Neno la Mungu kwa njia ambayo wanaweza kutoa Neno jipya kutoka kwa Bwana kwa ajili ya makusanyiko yao? Je, mlipuko wa upatikanaji wa zana umefanya iwe rahisi kwa viongozi wa Kikristo kulegeza viwango vyao wenyewe vya kusoma na kujinidhamisha, na kuwa watu wanaorudisha aina ile ile ya chakula walichopokea kutoka kwa wengine? Ni nani ambaye hajakutana na hadithi ya kijana mpendwa, mnyenyekevu, na mpole ambaye moyo wake uliwaka moto kwa ajili ya Bwana na mwenye matumaini ya kutumiwa naye, ambaye alikubaliwa kwa furaha katika seminari ya mbali au Chuo cha Biblia? Baada ya miaka takriban minne au mitano hivi, anarudi kwa ajili ya utumishi, na kugundulika kuwa namna yake ya kuhubiri na kufundisha imebadilika kabisa. Badala ya kujikita zaidi katika mambo aliyokuwa akisisitiza (k.m., kumpenda Mungu, shauku ya kuvuna roho za watu, kutafuta uwepo wa Mungu katika ibada, kufurahia kina na nguvu za Neno la Mungu, n.k.), sasa anataka kuzungumzia dhana ngumu za kitheolojia. Akitumia maneno na misemo ambayo inaweza kueleweka na watu wenye elimu zaidi katika kusanyiko, mafundisho yake siyo tena yale yaliyojawa na machozi na kumtamani Mungu bali ni mabishano kuhusu masuala ya kitheolojia ambayo yanaonekana kuwa madogo na yasiyo na umuhimu. Ni nini kilimpata ndugu yetu? Ni kwa njia gani kujikita katika zana, nyenzo, maarifa, na utaalamu kupita kiasi kunamfanya mtu mwenye moyo na mtazamo wa aina hiyo awe na kiburi na majivuno? Je, mtu anawezaje kufurahia na kutiwa nguvu na zana nyingi za kibiblia zilizopo bila kujivuna na kufanyika wa kuchosha na asiyezaa matunda katika mchakato huo? Maarifa yanapumbaza

1

4

2

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker