Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 1 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Hujakombolewa kwa sababu huijui ukweli

Hivi majuzi, mshirika wa kanisa moja la mjini alikerwa na washirika watatu wa Jumba la Ufalme laMashahidi wa Yehova waliokuwa wakitembeleamitaa anayoishi. Baada ya dakika chache za mazungumzo ya upole, walianzisha moja ya mada chokonozi zinazoambatana na hisia kali – kukana uungu wa Yesu Kristo. Mshirika huyo, mtu mwenye ujuzi mkubwa wa maandiko, alijitahidi kuutetea uungu wa Yesu kwa kadiri alivyoweza na kwa kiwango cha uelewa wake. Mashahidi hao watatu, hata hivyo, mara kwa mara walirejelea Kiyunani cha Yohana 1:1, ambacho walidai kuwa kilikosa kibainishi mahususi cha Kiyunani, na kufanya tafsiri nyingi katika tafsiri zetu za Kiingereza cha kisasa kuwa za uongo. Akiwa amechanganyikiwa na kufadhaika, mshirika huyo amemwomba mchungaji aandae darasa la awali la Kiyunani, ili aweze kutetea imani yake kuhusu Yesu kwa uhakika zaidi na kwa ushahidi bora zaidi. Ni jibu gani linafaa kujibu madai ya vikundi kama hawa Mashahidi, wanaodai kwamba imani nyingi za Kikristo hazitokani na ujuzi sahihi, bali ushirikina, mapokeo, na ujuzi wa uongo kuhusu Biblia? Tunapaswa kujitahidi kuwasaidia waumini wote kupata ujuzi bora wa lugha za Biblia, au kuzingatia zaidi masuala ya ukuzi na ukomavu wa kiroho? Matumizi ya lugha na zana za kitheolojia yana nafasi gani katika kuwapa washirika wetu uwezo wa kutumia kwa halali na kutetea vyema Neno la kweli kama lilivyo katika maandiko? Wengi wetu tumekuwa wahanga wa mazungumzo na mtu ambaye anataka kutukosoa katika kila kitu ambacho tumekiamini. Anapokuuliza ikiwa umewahi kusikia au la kuhusu msomi fulani mashuhuri wa Biblia, “Dakt. X,” anaanza kukueleza kwa nguvu na ushawisi mwingi namna ambavyo amebadilishwa na “ufunuo wake mpya” katika Neno la Mungu. Bila kujalisha “Dk. X” alizungumza kwa kina na ubobevu mkubwa kuhusu mada gani, sasa kwa rafiki yetu huyu, maneno ya “Dk. X” yamekuwa neno la uhakika juu yamada hiyo. Ukweli tu kwamba hujawahi kusikia kuhusu Dk. X na mafundisho yake ya kubadilisha maisha katika somo hilo ni kama unaonyesha namna ambavyo umetengwa na huna uelewa wa mafundisho ya hivi karibuni na bora zaidi ya Bwana kuhusiana na mada hiyo. Baada ya kusikiliza kwa muda mawazo ya Dk. X, unamaliza mazungumzo kwa upole iwezekanavyo. Baada ya kutafakari zaidi, unagundua kwamba mojawapo ya matatizo yanayotokana na kutafuta ujuzi mwingi ni uwezekano halisi wa kuzuka na kukua kwa kasi kwa uzushi mpya, madhehebu mapya, na mitazamo ya kiimani isiyo ya kawaida. Huku watu wengi sasa wakijinasibu kuwa wanafanya hayo chini ya uongozi na baraka za Mungu mwenyewe, maelfu ya walimu na wahubiri wote Hivi ni kweli kwamba kuwa na maarifa kidogo ni vibaya kuliko kutokuwa nayo kabisa?

3

4

4

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker