Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 1 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Ikiwa ungependa kujifunza kwa kina baadhi ya mawazo ya somo hili la Mafunzo ya Biblia: Kutumia zana za kujifunzia katika kujifunza Biblia , unaweza kujaribu vitabu hivi: Bruce, F. F. New Testament History . New York: Doubleday, 1969. Penney, Russell, and Mal Couch. eds. An Introduction to Classical Evangelical Hermeneutics: A Guide to the History and Practice of Biblical Interpretation . Grand Rapids: Kregel Books, 2000. Sire, James W. Scripture Twisting: Twenty Ways the Cults Misread the Bible . Downers Grove, IL: InterVarsity, 1980. Stott, John. The Contemporary Christian: Applying God’s Word to Today’s World . Downers Grove, IL: InterVarsity, 1992. Kuelewa njia ambazo zana hizi zinaweza kukusaidia zaidi kuelewa ulimwengu wa kale, kutakufanya kuwa mhudumu bora wa Neno la Mungu katika ulimwengu huu. Hakuna kitakacho boresha kila nyanja ya huduma yako kama kuwa mahiri katika Neno la Mungu. Lengo letu linapaswa kuwa sawa na Neno la Bwana kutoka kwa Paulo kwenda kwa Timotheo katika 2 Tim. 4:1-2 : “Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; 2 lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.” Mwanamume au mwanamke wa Mungu ambaye atajitia nidhamu katika Neno la Mungu, kuwa tayari kuhubiri, kufundisha, kusema, kushauri, na kuombea wengine wakati wowote ambao Mungu anaweza kumwelekeza, bila kujali mahali au mazingira, hana cha kupoteza. Hii ndio ndoto na jukumu letu! Sasa una fursa ya kushirikisha wengine maarifa ambayo umejifunza katika moduli hii kupitia mazoezi ambayo wewe na mkufunzi wako mtakubali. Kitakachokuwa muhimu ni kupata mahali ambapo unaweza kushirikisha maarifa tele ambayo umejifunza na kutumia katika moduli hii – iwe na watu wa familia yako, katika ukumbi kanisani kwako, kazini, au popote ambapo Mungu anaweza kuongoza. Unachopaswa kuzingatia ni kuhusianisha mafundisho haya na maisha yako, kazi, na huduma yako. Hilo ndilo kusudi la Kazi (mazoezi) ya huduma, na katika siku za usoni utakuwa na fursa ya kushirikisha maarifa haya katika maisha halisi na mazingira halisi ya huduma. Mwombe Mungu akupe ufahamu wa njia zake unaposhirikisha wengine maarifa haya kupitia zoezi hili.
Nyenzo na bibliografia
Kuhusianisha somo na huduma
4
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker