Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 1 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Sasa kwa kuwa uko mwishoni mwa moduli hii, tafakari kama kuna masuala yoyote, watu, hali, au fursa zilizosalia ambazo zinahitaji kuombewa kama matokeo ya masomo yako katika moduli hili. Mwombe Bwana, Roho Mtakatifu, akufunulie maombi au mabadiliko yoyote anayotamani kuyaona maishani mwako kutokana na masomo haya, na upate muda wa kuomba pamoja na wenzako kwa ajili ya maeneo yao yanayowahusu. Kumbuka, maombi hutupatia msaada tunaohitaji ili kufuatilia kwa imani na kwa ujasiri maeneo hayo ambayo Bwana wetu anatamani kuona mabadiliko na ukuaji.
Ushauri na maombi
KAZI
Hakuna kazi ya kukusanya.
Kukariri maandiko
Hakuna kazi ya kukusanya.
Kazi ya usomaji
Sasa unapaswa kuainisha mapendekezo yako kuhusu Kazi (mazoezi) ya Huduma na kuyakabidhi kwa mkufunzi wako ili aweze kuyapitia na kuyathibitisha. Hakikisha kwamba unajipanga mapema, ili usichelewe kukamilisha na kukusanya kazi zako.
Kazi nyingine
4
Mtihani wa mwisho utakuwa wa kufanyia nyumbani, na utajumuisha maswali yaliyochukuliwa kutoka katika majaribio matatu ya kwanza, maswali mapya kuhusiana na yale tulioyojifunza katika somo hili, na maswali ya insha ambayo yatakuhitaji kutoa majibu mafupi kwa maswali muhimu ya kuhusianisha maarifa haya na maisha na huduma yako. Pia, wakati wa mtihani, unahitaji kujiandaa kunukuu kwa kusema au kuandika aya zilizokaririwa katika kozi hii. Ukimaliza mtihani wako, tafadhali mjulishe mkufunzi wako na hakikisha anapata nakala yako. Tafadhali kumbuka: Matokeo yako na daraja lako la ufaulu katika moduli hii haviwezi kubainishwa ikiwa hutafanya mtihani wa mwisho na kukabidhi kazi zote zikiwa zimekamilika kwa mkufunzi wako (kazi ya huduma, kazi ya ufafanuzi, mistari ya kumbukumbu ya maandiko, Fomu za Ripoti ya Usomaji, majaribio, na mtihani wa mwisho). Katika somo hili tumeona aina za zana tunazoweza kupata ambazo zinaweza kuboresha kazi yetu ya kutafsiri Biblia. Tumezingatia hitaji la ufasiri wa kibiblia, na maandalizi yetu wenyewe ya mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu ili kulishirikisha kwa wengine Neno la milele la Mungu Aliye Hai. Tumechunguza mada ya uvuvio
Taarifa ya mtihani wa mwisho
Neno la mwisho kuhusu moduli hii
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker