Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 6 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
K I A M B A T I S H O C H A 2 5 Mtazamo wa Kristo Kuhusu Biblia Paul P. Enns. The Moody Handbook of Theology (Electronic Ed.). Chicago: Moody Press, 1997.
Katika kutambua asili ya uvuvio wa Biblia, hakuna ambacho kinaweza kuwa na umuhimu mkubwa sana zaidi ya kutambua mtazamo wa Kristo kuhusiana na Maandiko. Hakika hakuna yeyote anayeruhusiwa kuyatazama Maandiko kwa mtazamo wowote wa chini zaidi ya ule ambao Yesu alikuwa nao; mtazamo wake wa Maandiko ndio unatakiwa kuwa mtazamo wa kielelezo na wenye mamlaka kwa mitazamo ya watu wengine. Hiyo ndio hoja kuu ya Mwanathiolohia, Profesa R. Laird Harris. Katika kutetea uvuvio wa Maandiko hatumii Maandiko ya 2 Timotheo 3.16 au 2 Petro 1.21 kama Maandiko ya msingi kwa hoja hiyo, (ingawa anatambua uhalali wake); badala yake anatetea hoja kwa msingi wa mtazamo wa Kristo kuhusu Maandiko. (1) Kuvuviwa kwa kitabu chote. Katika kutumia kwake Agano la Kale Kristo alitoa uthibitisho kuhusu uvuvio wa Agano la Kale lote. Katika Mathayo 5.17–18 Kristo anathibitisha kwamba hakuna hata nukta wala yodi ambayo itaondolewa kutoka kwenye Torati hata yote yatimie. Katika msitari wa 17 alizungumzia Torati au manabii, kauli ya kawaida inayoelezea Agano lote la Kale. Katika kauli hii yenye nguvu, Yesu alithibitisha kutokuwa na makosa kwa Agano zima la Kale na hivyo akathibitisha uvuvio wa Agano zima la Kale. K atika Luka 24.44 Yesu anawakumbusha wanafunzi wake kwamba vitu vyote vilivyoandikwa kuhusu yeye katika torati ya Musa, manabii, na Zaburi lazima vitimie. Wanafunzi walishindwa kuelewa mafundisho kuhusiana na kifo na kufufuka kwa Kristo katika Agano la Kale, lakini kwa sababu ya kuvuviwa kwa Agano la Kale, yale matukio yaliyo tabiriwa yalitakiwa kutokea. Kwa kutoa kwake sifa za Agano la Kale, Kristo alikuwa anathibitisha kuvuviwa na mamlaka ya Agano zima la Kale. Y esu alipokuwa akishindana kwa hoja na Wayahudi wasioamini kuhusiana na haki yake ya kuitwa Mwana wa Mungu, aliwapeleka kwenye Zaburi 82.6 na kuwakumbusha “Maandiko hayawezi kutanguka” (Yohana 10.35). “ina maana kwamba Maandiko hayawezi kuondolewa nguvu yake kwa kuonyeshwa kwamba yamepotoka.” Ni lazima izingatiwe kwamba Yesu alinukuu hata Maandiko kutoka kwenye Agano la Kale ambayo kwa haraka yanaonekana kama hayana uzito sana na hivyo kuonyesha kwamba Maandiko hayawezi kutenganishwa au kubatilishwa.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker