Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 6 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Mtazamo wa Kristo Kuhusu Biblia (muendelezo)

(2) K uvuviwa kwa sehemu tu za Maandiko. Kristo alinukuu mara nyingi kutoka kwenye Agano la Kale. Hoja zake zilijikita zaidi katika ukamilifu wa Maandiko ya Agano la Kale aliyokuwa akinukuu. Kwa njia hii ya mijadala, Kristo alikuwa akithibitisha uvuvio wa sehemu moja moja au vitabu vya Agano la Kale. Mifano michache itatosha. Yesu alipokutana na Shetani katika kipindi cha jaribu lake, aliyashinda majaribu ya Shetani kwa kutumia kitabu cha Kumbukumbu la Torati katika Mathayo 4.4, 7, 10 Yesu ananukuu kutoka kitabu cha Kumbukumbu la Torati 8.3; 6.13, 16, akionyesha kwamba Shetani hakuwa sahihi na kusisitiza kwamba maneno haya yaliyoandikwa katika Kumbukumbu la Torati yalitakiwa kutimia. Katika Mathayo 21.42, Yesu alinukuu kutoka Zaburi 118.22, ambayo inafundisha kwamba Masihi atakataliwa. Katika Mathayo 12.18–21 Yesu alinukuu kutoka Isaya 42.1–4, akionyesha kwamba kufanya kwake amani, hali ya upole na ujumuishaji wa mataifa, yote yalishakuwa yametabiriwa zamani katika maandiko ya kinabii. Hii ni mifano tu michache tuliyoichagua, inayofunua kwamba Kristo alinukuu sehemu mbalimbali za Agano la Kale, akithibitisha uvuvio na mamlaka yake. (3) K uvuviwa kwamaneno.Katika kutetea fundisho la ufufuokwaMasadukayo, Yesu ananukuu kutoka kitabu cha Kutoka 3.6 (ni muhimu kwasababu Masadukayo walikuwa wanavishikilia vitabu vitano tu vya Musa), “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu.” Katika majibu haya, majibizano yote ya Yesu alijikita kwenye maneno “Mimi Niko.” Yesu alikuwa anatumia maneno hayo ambayo yalikuwa na yana maana sana kwa Maandiko ya kiebrania tu. Na hivyo alikuwa anaunga mkono Septuajinti (toleo la kiyunani la Biblia ya Kiebrania) toleo lililohusisha maneno hayo. Toleo hilo lilichukuliwa na wengi waliokuwepo nyakati za Bwana Yesu kwamba lilikuwa linawekwa katika hadhi sawa na Maandiko ya asili. K atika kuthibitisha ufufuo, Yesu aliwakumbusha Masadukayo, kwamba Kut 3.6 inasema “Mimi niko.” Akaelezea: “Mungu si Mungu wa wafu bali ni Mungu wa walio hai.” Kama maneno ya Agano la Kale hayakuwa yamevuviwa, basi hoja zake zilikuwa ni bure; lakini kama maneno yale yalikuwa yamevuviwa basi hoja zake zinabeba uzito mkubwa. Kwa kweli, mjadala wa Yesu unajikita kwenye wakati uliopo wa kauli ile. Kwa sababu iliandikwa kwenye kitabu cha Kutoka 3.6 “Mimi niko.…”, fundisho la ufufuo linaweza kuthibitishwa; Mungu ni Mungu wa mababa wa imani walio hai. M fano kama huo unapatika katika Mathayo 22.44 ambapo Yesu anabishana na mafarisayo kwamba mtazamo wao juu dhana ya Masihi ulikuwa sio sahihi. Mafarisayo walimfikiria Masihi kama mkombozi wa kisiasa lakini

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker