Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 6 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Mtazamo wa Kristo Kuhusu Biblia (muendelezo)
Yesu anawaonyesha kutoka kwenye nukuu yake katika Zaburi 110.1 kwamba Daudi, Mfalme mkuu zaidi wa Israeli alimuona Masihi kama mkuu zaidi yake yeye, hata akamwita Bwana. Mjadala wote wa Kristo unaelezea kuhusu neno “Bwana wangu”. Katika kunukuu Zaburi 110.1 Yesu aliweka hoja yake katika uvuvio wa maneno mafupi “Bwana wangu”. Kama Zaburi 110.1 haikuwa inasomeka “Bwana wangu” basi hoja zote za Yesu zilikuwa hazina nguvu. Mfano wa nyongeza ni Kristo kutumia Zaburi 82.6 katika Yohana 10.34 ambapo hoja zake zote zinalenga katika neno “miungu”. (4) K uvuviwa kwa hefuri. Katika idadi kubwa ya kauli zake Kristo anaonyesha kwamba aliamini kwamba herufi za Maandiko zilikuwa zimevuviwa. Katika Mathayo 5.18 Yesu anatangaza “Hakuna hata nukta wala yodi ambayo itapita mpaka yote yatimie.” Neno “herufi ndogo” lina maanisha katika Kiebrania yodi, ambayo inaonekana kama funga semi(‘) na nukta inamaanisha utofauti mdogo sana uliopo kati ya herufi mbili za kiebrania. Utofauti unaweza kuwa ni sawa na ule uliopo kati ya herufi O na Q kamkia kadogo tu ndio kanakotofautisha Q kutoka kwenye O. Yesu aliendelea kusisitiza kwamba yote yaliyoandikwa katika maandiko ya Agano la Kale yatatimizwa katika hatua zote, mpaka herufi ndogo kabisa. (5) U vuvio wa Agano Jipya. Katika mazungumzo yake kwenye chumba cha juu, Kristo alisema kauli ambayo inalenga kuonyesha ukuu na usahihi wa Maandiko ya Agano Jipya. Katika Yohana 14.26 Yesu aliashiria kwamba Roho Mtakatifu angewakumbusha kikamilifu mitume pale wanapo andika maneno ya Maandiko, hivyo kuonyesha usahihi wake ( ling. Yohana 16.12-15). Hii inaweza kuelezea ni kwa namna gani mtu mzee kama Yohana anapoandika maisha ya Kristo anaweza kuelezea kwa kina kila taarifa ya matukio ambayo yalitukia miaka mingi iliyopita kabla. Roho Mtakatifu alimpa Yohana na waandishi wengine kumbukumbu yenye nguvu ya kukumbuka. Hivyo, Yesu hakuthibitisha tu uvuvio wa Agano la Kale lakini pia Agano Jipya. Hitimisho lisilo na shaka ni kwamba Yesu alikuwa na mtazamo wa juu sana kuhusiana na Maandiko, akithibitisha uvuvio wake katika Agano la Kale lote – vitabu mbalimbali vya Agano la Kale, maneno yaliyomo na herufi zake – na alithibitisha uvuvio wa Agano Jipya. Hakika wale wanaoona kama uvuvio upo katika dhana fulani tu au kutofautiana na hayo wanahitajika kutazama upya mtazamo wa Yesu katika Maandiko. Je mtazamo wake hautakiwi uwe ndio kipimo? Je ni sawa kuwa na mtazamo wa chini kuhusiana na Maandiko kuliko ule aliokuwa nao yeye?
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker