Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

2 6 8 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Hadithi, Theolojia, na Kanisa (muendelezo)

Hoja ya Tatu: Hadithi daima zina mamlaka.

Tumeona katika sura ya kwanza ya kitabu hiki kwamba kila theolojia ni akisi ya hadithi za asili. Ili kupima theolojia, lazima mara zote turudi nyuma kwenye maandishi ya kale (na namna kulivyokuwa kuenea kwake baadae). Kwa kiwango hiki hadithi za Biblia zitabaki ziku zenye mamlaka. Kuna tahadhari kubwa sana, hata hivyo, wengine wanaweza kurudi nyuma na kutengeneza vinyago kutoka kwenye hadithi hiyo; kwa maana kwamba wanaweza wakachukulia kama maandishi ambayo yako hivyo siku zote, wakayatoa kutoka katika historia, kuja kwenye ulimwengu huu na kuyalazimisha kubaki katika hali ileile ya mwanzo. Hili ni tatizo la wafasiri wanachukulia maandiko kama yalivyo na wafuasi wakihafidhina wa misingi ya kale. Mapokeo yanatokea kutoka kwenye hadithi. Hiyo ndio asili ya hadithi ya muhimu na yenye mantiki. Watu “wakivutiwa” na hadithi, shujaa wake au adui wake na ujumbe wake, hawatamani tu kushirikisha uzoefu bali kushirikisha uzoefu ulio sawasawa na hadithi ya asili. Hivyo mapokeo yanachipuka ambayo yanakuwa na kazi mbili: Kuhifadhi na kulinda. Kuhifadhi ni “Kukabidhi kwa wanaofuata” ambacho ndicho neno mapokeo lina maanisha moja kwa moja. Kulinda kunaweza kuhitaji maelezo zaidi kidogo. Kwa sababu hadithi hakika ni sitiari zilizopanuka zaidi, huwa mwisho wake bado unaruhusu mawazo zaidi. Zinaweza kubadilika na kubadilisha wahusika na usimulizi wake kirahisi. Taarifa majina, na maeneo yanaweza kuchukuliwa tofauti kwa hadhira na maeneo tofauti. Tunaligundua hili hata katika kipindi kifupi cha uandishi wa vitabu vinne vya Injili. Hata hivyo mpaka umewekwa ili kuzuia mtu kwenda mbali zaidi lakini bado akawa sahihi kabisa kutokana na hadithi wa awali. Tukichuchukua mifano ya kidunia: Santa Claus anaweza kubadilika kwa karne zote kirahisi zaidi. Anaweza kuwa mrefu au mfupi, mwenye uso mwanana au wenye mikunjo, aliyevaa nguo za zambarau au kijani, mnene au mwembamba kama muigizaji wa nafasi ya Ichabod Crane. Lakini Santa hawezi kamwe kuwa mnyanyasaji wa watoto. Ukizingatia kwamba alipokea kutoka kwa Mt. Nicholaus, aliyepokea kutoka kwa mtoto Yesu, aliyepokea kutoka kwa Baba wa vipawa vyote. Mapokeo ya asili yasingeweza kuruhusu uhusiano baina ya Santa na madhara yoyote wakati lengo lake kubwa ni wema na ukarimu. Katika kuendelea na hayo kuna sehemu mapokeo yangeilinda sura hiyo kutoka kwenye mkanganyiko. Hadithi za Biblia Hoja ya Nne: Mapokeo yanatokea kutoka kwenye hadithi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker