Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 6 9

K U T A F S I R I B I B L I A

Hadithi, Theolojia, na Kanisa (muendelezo)

kuhusu Yesu zinahimiza mchakato huohuo wa kulinda. Hapa ndipo Mapokeo ya Kanisa yanaingia. Na kwasababu hadithi za Yesu zinatofautiana, basi mapokeo yanayotofautiana sio tu yatachipuka lakini pia yatakuwa halali kabisa.

Hoja ya Tano: Hadithi hutangulia na kuzalisha kanisa.

Hili tulilitazamaMwanzoni.Hadithi inakuwepokwanzanakishawatuwanashawishiwa nayo, wanatazama uzuri wake, wanaitafakari, wanaihadithia upya, wanaihifadhi na kuisema kwa watu wengine (mapokeo) pale ambapo watu wengi wanakuwa wameshawishiwa nayo, wameiamini na kuifurahia, hapo sasa una Kanisa.

Hoja ya sita: Hadithi inamaanisha laumu.

Hoja hii ni matokeo ya kimantiki ya hoja mbili zilizotangulia: Kama una mapokeo ambayo yamejikita katika kuhifadhi na kueneza kiini cha hadidhi husika, na kama una Kanisa linaloishi sawasawa na hiyo na kusherekea hiyo hadithi kuu, basi wale walio katika kundi ambalo muda wowote linaweza kwenda kinyume kwa kiwango kikubwa na hadithi ya msingi ni lazima washughulikiwe. Hapa ni sehemu ya kawaida sana katika maisha yote. Hapa ndipo tunapata dini, serikali, au shutuma, karipio, na kutengwa. Uwanja mpana unaruhusiwa lakini siyo kwenda mpaka hatua ya kukinzana na kile ambacho hadithi inakisimamia. Makundi yenye msimamo hayawezi, kwa mfano, kuvumilia upinzani uliopitiliza. Bila shaka, kama historia ilivyoonyesha watu huwa wanakuwa wanajizuia sana kwa kile wanachokiamini kuwa mapokeo ya “Kweli” kuliko hali yake ya kuwa sahihi au la. Fundisho la msingi kwa mtu mmoja linaweza kuwa uzushi kwa mtu mwingine kutegemeana na nani ana mamlaka kuu zaidi. Lakini hilo sio hoja kubwa hapa. Hoja hapa ni kwamba pale ambapo hadithi inachipuza mapokeo, na mapokeo yakachipuza Kanisa, basi shutuma katika maeneo fulani inatokeza muda wowote. (Kimsingi, mapema sana kama tulivyoona katika kujifunza kutoka katika nyaraka za Paulo). Katika Mapokeo yetu ya kikatoliki hiki ndicho chanzo cha adhabu na kutengwa.

Hoja ya Saba: Hadithi zinazalisha theolojia

Tafakuri na hitimisho kutoka katika hadithi za Yesu zilianza mapema sana katika Kanisa. Tunaliona hili katika Maandiko ya Mwanzo kabisa ya Kanisa, nyaraka za Paulo. Pale unapotafakari juu ya hadithi, unganisha matukio na kupata

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker