Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 7 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Hadithi, Theolojia, na Kanisa (muendelezo)
hitimisho,hapo tayari una theolojia. Tunaweza kuona hili kirahisi, kwa mfano katika njia ya imani kuhusiana na asili ya Yesu. Kwa namna ya kipekee sana hadithi inatuambia yeye ni mtu wa Mungu. Kama ni mtu wa Mungu basi labda yeye ndiye msemaji wake pia na labda yeye ndiye Neno lake. Na kama yeye ni Neno lake basi labda anauhusiano maalumu na Baba, na kama anauhusiano maalumu na Baba, labda yeye ni Mwana wake-kwa namna ya kipekee. Na kama ni Mwana wa Mungu, labda yuko sawa naye. Na kama yuko sawa naye labda yeye ni Mungu katika mwili. Theolojia ni kuweka vipande vidogo vidogo pamoja na kugundua hitimisho lenye mantiki zaidi kuliko lile ambalo lingeweza kufikiwa mwanzo. Au tunaweza kuiweka kwa namna hii: Theolojia inachipuza kwa sababu mara zote huwa kuna vitu vya zaidi katika hadithi kuliko vile ambavyo msimuliaji ama amevigungua au amekusudia kusimulia. Tuna mfano halisi katika kitabu cha Injili ya Yohana (11.49-52): “Mtu mmoja miongoni mwao, kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka ule,akawaambia ‘ninyi hamjui neno lolote; wala hamfikiri ya kwamba ya faa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu, wala lisiangamie taifa zima’, kisha Yohana anaendelea na kutoa tafakari yake na maana zaidi kuhusiana na maneno haya (theolojia): “Na neno hilo yeye hakulisema kwa nafsi yake; bali kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri ya kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa hilo, wala si kwa ajili ya taifa hilo tu; lakini pamoja na hayo awakusanye watoto wa Mungu waliotawanyika, ili wawe wa moja”. Wakati na kutazama yaliyotangulia mara nyingi kunafunua mawazo muhimu zaidi katika hadithi. Theolojia inashikilia hili na inalifunua. Theolojia ina mizizi yake na inaenda sawa na hadithi. Hadithi za Yesu zenyewe zinatofautiana na bila shaka zina akisi mapokeo tofauti. Hata usomaji wa kawaida wa vitabu vinne vya Injili unaonyesha hili. Na kwasababu hili liko hivyo, basi tunatarajia mapokeo hayo tofauti ya hadithi yatatupa aina mbalimbali za theolojia. Hakuna mfumo mmoja uliotengenezwa ili kwamba uwe ndio huo tu. Hadithi za kawaida zenyewe, ambazo pia, sio tu zinaruhusu mawazo zaidi mwishoni bali pia zimewekwa katika hali ya dhana na katika marejeo ya mfumo wa nyakati zake. Kumekuwa na kutaendelea kuwa na mifumo mingi ya theolojia katika Kanisa. Ingawa kumekuwa na msukumo katika nyakati hizi za sasa wa kuifanya mifumo yote iwe mmoja, katika historia ya Kanisa kumekuwa na uvumilivu sana juu ya utofauti uliopo katika mifumo hii. Hoja ya Nane: Hadithi zinazalisha theolojia nyingi.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker