Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook

/ 2 7 1

K U T A F S I R I B I B L I A

Hadithi, Theolojia, na Kanisa (muendelezo)

Hoja ya Tisa: Hadithi zinatengeneza ibada na sakramenti

Lazima tukumbuke kwamba maisha ya Yesu yalianza kabla ya tafakari kumhusu yeye. Hii ndio njia ya kuhifadhi maisha hayo ambayo yalikuwepo kabla ya kuyafikiri, na hadithi hiyo ilikuja kabla ya theolojia. Maisha ya Yesu yalikuwa halisi, kama tulivyoona, yakiwekwa katika hadithi, lakini ni lazima pia izingatiwe kwamba yaliingizwa sambamba katika sherehe za kidini na sikukuu mbalimbali. Ishara, matendo, utumiaji wa lugha ya mwili na alama pia zilikuwa sehemu ya hadithi nzima. Sherehe ya ibada yenyewe ni sehemu ya hadithi katika matendo. Hivyo kutokea hapo zilitokea desturi za kidini zinazoigiza upya kifo, mazishi na ufufuo wa Yesu. Paulo anauita huu kuwa ni ubatizo. Na kisha kulikuwa na mlo wa kiibada wa kuumega mkate na kukinywea kikombe, ishara za matendo ya kutolewa kwa Yesu. Kiufupi, kulikuwa pia na hadithi ambazo watu waliziishi na kusimuliana mmoja na mwingine, ambazo tumekuja kuzieleza kama ni kushangilia kwa siri na mambo ya ajabu ya Mungu au zimekuja kuitwa tu sakramenti. Hadithi (neno) sherehe(tafrija) na ibada (sakramenti) zote zinakwenda pamoja. Bila shaka inaweza kutokea, na imeshatokea kwamba ibada inaweza kupoteza muunganiko wake wa hadithi, kupitia kufanyika kama taratibu za kawaida, kuboa, na kurudia mara kwa mara. Hii ikitokea watu kiuhalisia wanaendelea na ibada hizo kutokana na mazoea, lakini, hawakumbuki hadithi ilikuwa imeshikamana na nini au inaelezea nini. Ili kuhuisha au kuingiza upya matukio katika ibada hizi za kidini, lazima turudi nyuma na kukumbuka vizuri hadithi hiyo. Kufanywa upya kwa Kanisa kimsingi ni moja ya mazoezi ya kulikamilisha jambo hili.

Hoja ya Kumi: Hadithi ni historia

Kwa sababu hadithi zinamwisho unaoruhusu mawazo zaidi, zenyewe haziwezi kuwa au hazitakiwi kuchukuliwa kama zilivyo neno kwa neno. Hadithi zina uhai wa aina yake na kila kipindi kinatoa au kuongeza uhai huo kwa njia ya kuwa pamoja na kuhusiana. Matokeo yake ni kuwa na utajirisho wa kina. Historia ni daraja ambalo kwa hilo tunaitazama hadithi kutoka katika aina zake zote na katika masuala yake yote ya kweli. Kimsingi, historia inaiokoa hadithi kutoka katika hatari ya ibada ya sanamu na kutokuwa na umuhimu tena.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker