Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 8 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
K I A M B A T I S H O C H A 3 0 Orodha Hakiki ya Vipengele vya Simuli (Hadithi) Imetolewa kutoka kwa Mtaalamu wa lugha, Profesa Leland Ryken. Namna ya Kusoma Biblia kama Fasihi.
I. Muktadha wa Hadithi ni Ukoje?
A. Mazingira yanayozunguka B. Mazingira ya kihistoria C. Hali ya kiutamaduni D. Mahusiano kati ya mtu na mtu na mazingira yao
II. Akina nani ni Wahusika katika Hadithi?
A. Akina nani ni wahusika wakuu au wahusika wasaidizi katika hadithi? B. Nani ni “shujaa?” nani ni “adui”? C. Ni kwa namna gani mwandishi anaelezea ukuaji wa muhusika? D. Nini matokeo ya mwisho ya maisha na machaguo ya muhusika?
III. Ni Migogoro Gani ya Kisa husika Iliyopo katika Hadithi?
A. Nini migogoro mikuu na Mungu? B. Nini migogoro mikuu na watu wengine?
C. Nini migogoro mikuu kati ya wahusika wao wenyewe? D. Nini ni migogoro mikuu kati ya wahusika na hali zao?
IV. Ni Vipengele vipi vyenye Mafumbo ya katika Simulizi ambavyo Vimejifunua kwenye Hadithi? A. Nini kinatushawishi sisi tuweze kuwahurumia wahusika? B. Nini kinazalisha karaha na chuki kati yetu na wahusika? C. Nini kinatupelekea kukubaliana na kile ambacho wahusika wamefanya?
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker