Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 9 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
E. Soma Maandiko hayo katika tafsiri nyingine ya Maandiko.
Zana ya msingi: Tafsiri au matumizi ya maneno tofauti ya Maandiko kwa namna nyingine ambako kunatumia falsafa tofauti ya tafsiri na lile toleo la Maandiko ambalo unalitumia mara nyingi. • Andika swali lolote ambalo tafsiri hii mpya imeliibua akilini mwako na uwe makini katika kupata majibu yake unapoendelea kujifunza zaidi. F. Soma andiko la namnamoja na hilo kutoka katika sehemu nyingine za Maandiko. Zana ya msingi: Konkodansi na/au Biblia yenye marejeo. • Zingatia taarifa gani zimeongezwa kwenye kifungu unachosoma kutoka katika sehemu nyingine za Maandiko. • Kwanini mwandishi alichagua kuondoa baadhi ya taarifa na kuzisisitiza nyingine? Na hii ina faida gani kwa kuelewa dhumuni la mwandishi? Zana za Msingi: leksimu za Kiebrania na Kiyunani na Kamusi zenye mafafanuzi zinasaidia kuongeza kina cha uelewa wetu wa maana za maneno na matumizi yake. Vitabu vya Mafafanuzi ya Kieksejesia vinasaidia kuelezea muundo wa kisarufi na namna unavyoathiri maana ya andiko. • Zingatia maneno ambayo yametumika katika njia ya kipekee na mwandishi na aina ya namna anavyoitumia sarufi kama vile vitenzi au maneno yanayoonyesha ulazima wa jambo, vitenzi vinavyoonyesha tukio linaloendelea n.k G. Jifunze maneno na muundo wa kisarufi
H. Tambua tanzu (aina ya fasihi) na zingatia kanuni maalum zinazotumika kwa tanzu husika. Zana za msingi: Kamusi ya Biblia na kitabu cha Mafafanuzi ya Biblia
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker