Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 9 1
K U T A F S I R I B I B L I A
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
• Kila aina ya fasihi lazima ichukuliwe kwa uzito kwa vile ilivyo. Hatutakiwi kutafsiri ushairi kwa namna moja na tunavyo tafsiri unabii, au masimulizi kwa namna moja na kauli za amri.
I. Tafuta miundo ya fasihi ambayo inaweza kuathiri namna andiko linavyoeleweka. Zana ya msingi: Kitabu cha Mafafanuzi ya Kieksejesia • Muundo wa kifasihi unahusisha tamathali za semi, sitiari, mifano, alama, muundo wa kishairi, muundo wa tungo mfuatano n.k J. Tambua matukio ya kihistoria na masuala ya kitamaduni ambayo yangeweza kuathiri watu au kuathiri mawazo kwa namna yalivyoelezewa katika kifungu cha Maandiko. Zana za msingi: Kamusi ya Biblia na kitabu cha mafafanuzi ya Biblia • Mara zote jiulize, “nini kilikuwa kinatokea katika historia na jamii ambacho kingeathiri namna ambavyo hadhira iliuelewa ujumbe katika andiko hili?” K. Andika kwa ufupi kile ambacho unaamini mwandishi alikuwa anajaribu kusema na kwanini kilikuwa ni muhimu kwa hadhira ile ya asili. • Lengo lako katika hatua hii ni kuandika kweli za msingi za kifungu cha maaandiko kwa namna ambayo mwandishi na wasikilizaji wa asili wangeweza kukubaliana nazo kama wangezisikia.
Shabaha ya hatua hii ni kutambua ujumbe mkuu, kauli za amri, na kanuni katika sehemu ya Maandiko ambayo inafundisha kusudi la Mungu kwa watu wote.
Hatua ya Pili: Kutafuta Kanuni za Jumla
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker