Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
2 9 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
A. Orodhesha kwa muundo wa sentensi zile unazoamini kuwa ndio kanuni za jumla katika kifungu cha Maandiko na zinafaa kutumika kwa watu wote, wakati wote, katika tamaduni zote.
B. Lingamisha kauli hizi na sehemu nyingine za Maandiko kwa ajili ya uwazi na usahihi. Zana za msingi: Konkodansi, Biblia ya Mada Jiulize: • Kanuni nilizoziainisha zinakubaliwa na vifungu vingine vya Maandiko katika Biblia? • Ni zipi kati ya kanuni hizi zinaweza kuwa ngumu au haiwezekani kuzielezea pale zinapolinganishwa na vifungu vingine katika Maandiko? • Je, kuna kanuni yoyote kati ya hizi ambayo ni lazima ikataliwe kwa kuzingatia vifungu vingine vya Maandiko? • Ni taarifa gani mpya kuhusu Mungu na mapenzi yake kifungu hiki kinaongeza kwenye uelewa wangu wa jumla wa Maandiko na fundisho la imani? C. Boresha au rekebisha kauli zako za kanuni za kimungu kulingana na ugunduzi ulioufanya hapo juu. • Andika upya kanuni yako ya msingi kuakisi maarifa yaliyopatikana kutoka sehemu nyingine za Maandiko. D. Soma Vitabu vya Mafafanuzi ya Biblia ili kugundua baadhi ya kanuni za msingi na mafundisho ambayo wengine katika Kanisa wameyapata kutoka katika kifungu hicho cha Maandiko. • Linganisha na tofautisha taarifa kutoka kwenye mafafanuzi na kujifunza kwako binafsi. Uwe tayari kuziacha, kubadilisha, au kutetea mtazamo wako kila unapopata taarifa mpya.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker