Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 2 9 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Funguo kwa Utafsiri wa Biblia (muendelezo)
E. Kwa mara nyingine tena, rekebisha au boresha kauli zako za kanuni za kimungu kulingana na ugunduzi ulioufanya hapo juu.
Shabaha kubwa katika hatua hii ni kuhama kutoka kile ambacho Maandiko “yalimaanisha” Mpaka kile ambacho Maandiko “yana maanisha” leo. Je utii kwa sheria na kusudi la Mungu unaonekanaje kwa nyakati hizi katika utamaduni wetu, na familia na marafiki zetu, pamoja na matatizo na fursa tunazokumbana nazo katika maisha yetu? A. Muombe Mungu aongee nawe na akufunulie maana ya kifungu hiki cha Maandiko kwa ajili ya maisha yako. • Tafakari juu ya kifungu hicho cha Maandiko na vitu ulivyojifunza kutokana na usomaji wako huku ukimuomba Roho Mtakatifu kukuonyesha maeneo mahususi ya kutendea kazi hizo kweli zilizogunduliwa kwa ajili yako na wale wanaokuzunguka. B. Ni kwa namna gani kifungu hiki cha Maandiko ni “habari njema” Kwangu na kwa wengine? • Ni kwa namna gani kinamfunua Yesu na ufalme wake ujao? • Ni kwa namna gani kinahusiana na mpango mkuu wa Mungu wa ukombozi? C. Ni kwa namna gani kujua kweli kutoka kwenye kifungu hiki cha Maandiko: Kuna athiri mahusiano yangu na Mungu? • Jaribu kutambua ni kwa namna gani kanuni na mifano kutoka katika Maandiko haya vinakusaidia wewe kumpenda Mungu na kumtii kwa ukamilifu zaidi.
Hatua ya tatu: Kuzitendea kazi Kanuni za Jumla Leo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker