Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Student Workbook
/ 8 7
K U T A F S I R I B I B L I A
c. Angalia maelezo ya kifungu (ona Oletta Wald “Muhtasari wa Mbinu ya Hatua Tatu” katika sehemu ya kwanza ya somo hili).
3. Nyenzo hizi zinapaswa kusomwa ili kupata taarifa za msingi kuhusu muktadha halisi wa kwanza wa andiko, sio kwa ajili ya kupata tafsiri ya andiko.
C. Ni nani alikuwa mwandishi wa kitabu na tunajua nini kumhusu: Mtume Paulo.
1. Alikiandika pamoja na Sosthene, ndugu katika Korintho, 1 Kor. 1:1-2.
2
2. Kulikuwa na migawanyiko katika kutaniko kuhusiana na yeye, 1 Kor. 1:12-13.
3. Alijiona kuwa mtumishi aliyetumwa na Bwana kuhubiri Injili, 1 Kor. 3:4-5.
4. Alijihisi kuwa zawadi kwa kanisa la Korintho, 1 Kor. 3:22.
5. Salamu zake binafsi zimejumuishwa kwenye hitimisho la kitabu, 1 Kor. 16:21.
D. Hadhira yake ilikuwa ya watu gani, waliishi wapi, na walikuwa na shida gani? (mambo ya kiutamaduni na kihistoria).
1. Mji uliitwa “kituo cha dhambi” cha Dola ya Kirumi katika wakati wa Paulo.
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker