Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 0 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
kielelezo cha utendaji wa haki katika ulimwengu. Kupitia maisha na utume wa Kanisa, kwa uweza wa Roho Mtakatifu, Watu wa Mungu leo wanaonyesha na kufurahia shalom ile ile inayozungumzwa katika Agano la Kale. • Kanisa linaitwa kuonyesha ukarimu wa hali ya juu kwa wahitaji, kwa kuwapa kipaumbele cha pekee wale walio ndani ya jamii ya waaminio, hasa wajane, yatima na maskini. Pia tunawajibu wa kutoa misaada kwa makanisa mengine wakati wa misiba na dhiki. • Kama mwili wa Kristo ulimwenguni, Kanisa limeitwa kuwa mtetezi wa maskini, ambayo ni alama ya utume halisi wa Kikristo. Utetezi huu unajumuisha kutenda haki (yaani, kutokuwa na ubaguzi wala upendeleo kwa sababu ya tabaka au utofauti) katika mwili, kutenda matendo mema kwa niaba ya maskini na walio hatarini, na kufanya kazi ili kusaidia kukidhi mahitaji halisi ya wengine, hasa wale walio katika nyumba ya Mungu. • Kuhusu utume wa mijini, Kanisa limeitwa kutangaza Habari Njema kwa maskini, hilo ni pamoja na kuwaheshimu kama walivyochaguliwa na Mungu na kama watu ambao Kristo alijitambulisha nao. Hatupaswi kamwe kuwadhalilisha, bali kushughulika nao kwa haki na huruma, tukiwa na uhakika kwamba wanaweza kugeuzwa na kuchangia katika maendeleo ya Ufalme. • Kanisa lazima litende kwa kuzingatia kwamba Mungu amewachagua maskini. Hilo linamaanisha kwamba lazima Kanisa litetee maslahi yao, lidumishe haki zao, na kutoonyesha upendeleo katika mambo yetu katika Kanisa. Tunapaswa kuwa wakarimu katika kukidhi mahitaji ya maskini, kugawana mali zetu, kuwafadhili wageni na wafungwa, na kuonyesha upendo kama tulivyoonyeshwa. • Katika utoaji wetu wote na kujali kwetu, tunapaswa kutafuta haki na usawa kwa maskini, popote tunapowapata. Hatutakiwi kukidhi mahitaji yao kijuujuu tu, bali kujitahidi kushughulika na mifumo na mahusiano kwa namna ambayo itachochea hali ya haki zaidi, yaani kuishi “Injili ya mafanikio” ya kweli, ambayo ni kutafuta haki na usawa kwa niaba ya walio hatarini zaidi miongoni mwetu.
4
Made with FlippingBook - Online catalogs