Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 0 2 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

I. Yesu na kuanzishwa kwa Kanisa: Jamii ya Ufalme wa Mungu ya Agano Jipya

Muhtasari wa Sehemu ya Pili ya Video

Kanisa la Awali la Kikristo Liliundwa na Watu Maskini

Suala la kuwatunza maskini lilikuwa jukumu ambalo liliwekwa juu ya Paulo na Barnaba kwa makubaliano yao na Yakobo, Petro na Yohana (Gal. 2:10). Maskini miongoni mwa Wayahudi wa Kikristo huko Yerusalemu walihitaji kupewa misaada kwa ajili ya mahitaji yao, na Wakristo wa Mataifa walikuwa na wajibu kwao kama namna ya kutambua baraka za kiroho walizopokea kutoka Yerusalemu (Rum. 15:26-27). Changizo hilo limetajwa katika barua zote kuu za Paulo; analihimiza sana kanisa la Korintho kushiriki kutoa michango hiyo (1Kor. 16:1-4; 2Kor. 8-9). Sababu ya changizo husika ni hitaji la kijamii lililokuwepo miongoni mwa Wakristo huko Yerusalemu, ambalo kuna uwezekano kwamba lilisababishwa na uadui na mateso kutoka kwa jamii pana ya Wayahudi. Changizo hilo pia lilikuwa na kusudi la kisiasa kama ishara ya upendo na mshikamano kutoka kwa makanisa yaliyoanzishwa na Paulo. Wengi wa washirika katika makanisa ya Paulo walikuwa watu maskini wenye asili ya maisha ya chini (1 Kor. 1:26-28), lakini Paulo anasisitiza utele ambao walikuwa wameupokea kupitia Injili, ‘kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote’ (2 Kor. 6:10). Katika kuhimiza ushiriki wao katika changizo hilo Paulo pia anafafanua juu ya maana pana ya maneno ‘tajiri’ na ‘maskini’. Katika 2 Wakorintho 8:9 Kristo ‘tajiri’ amekuwa ‘maskini’ – akirejelea suala la Yesu kuvaa mwili (rej. Flp 2:6) – ili waamini waweze kuwa matajiri na kushirikiana wao kwa wao. Kristo anatoa kiwango kipya cha maadili (Flp. 3:8), na hazina ya Injili inajenga ukarimu katika kuwafadhili wahitaji (1 Tim. 6:17-19). ~Hans Kvalbein. “Poverty.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, mh. (toleo la kielektroniki). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2001 .

4

A. Moyo wa Mungu unafunuliwa kupitia uzinduzi wa huduma ya Yesu pale anapotangaza umasihi wake (hotuba ya Yesu ya uzinduzi huko Nazareti), Luka 4:16-21.

1. Yesu ndiye Masihi ambaye huduma yake inazinduliwa kwa upako kutoka kwa Mungu ili kuwahubiria maskini . Yoh 1:41: “Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).”

Made with FlippingBook - Online catalogs