Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 0 3
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
2. Ni upako wa haki, Zab. 45:7, taz. Ebr. 1:9.
3. Mfalme ajaye angekuwa mpenda haki na usawa, Zab. 99:4.
4. Yesu alihubiri Habari Njema ya msamaha na amani kwa maskini, Luka 6:20.
5. Unabii wa Kimasihi ulizungumza juu ya Yule ambaye angewafanya maskini wa wanadamu washangilie katika Mungu, Isa. 29:19-20.
6. Huduma kwa maskini ni uthibitisho usiopingika wa umasihi wa Yesu .
a. Msingi wa mwelekeo wa huduma yake: Maandiko mahususi aliyo chagua (Mtumishi wa Kimasihi).
4
b. Msingi wa wito wake: upako wa Roho Mtakatifu.
c. Walengwa wa huduma yake: maskini, mateka, vipofu, walioonewa.
d. Msingi wa kusudi lake: kutangaza mwaka wa neema ya Bwana.
B. Yesu anathibitisha umasihi wake kwa Yohana Mbatizaji kupitia matendo ya haki na kuwahubiria maskini, Luka 7:18-23.
1. Mashaka ya Yohana Mbatizaji: wewe ndiwe yule ajaye, au tumtazamie mwingine? , mst. 19.
Made with FlippingBook - Online catalogs