Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 0 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

2. Jibu la Yesu: aliponya magonjwa na matatizo mengi, alifukuza mapepo, akaponya vipofu.

3. Mtindo wa Yesu ni wa “onyesha-na-sema”: Nendeni mkamweleze Yohana hayo mliyoyaona na kuyasikia; vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanahubiriwa habari njema (mst. 22).

4. Dalili za wakati wa mwisho na udhihirisho wa Ufalme uliopo: Ishara za Yesu ni uthibitisho usiopingika kwamba yeye ndiye Masihi wa Maandiko ya Kiebrania!

5. Huduma kwa maskini ni uthibitisho usiopingika wa utambulisho wa Masihi.

C. Yesu anahakiki na kuthibitisha wokovu wa watu kwa jinsi wanavyowatendea maskini, Luka 19:1-9.

4

1. Zakayo kama msaliti wa jamii ya agano: mwaminifu kwa utawala wa Kirumi na mnyang’anyi wa watu wa Mungu (yaani, mtoza ushuru tajiri ).

2. Kukutana kwake na Yesu Kristo na udhihirisho wa wazi wa badiliko la moyo.

a. Nusu ya mali yangu ninawapa maskini (ishara badiliko la kweli la moyo).

b. Ikiwa nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, ninamrudishia mara nne (ukarimu wa hali ya juu na urejeshaji).

Made with FlippingBook - Online catalogs