Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 0 5
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
3. Ukarimu wa Zakayo si njia ya kupata wokovu, bali ni uthibitisho wa wokovu, taz. 1 Yoh. 4:7-8; 1 Yoh. 3:16; Yak. 2:14-16.
4. Jibu la Yesu: Leo wokovu umefika nyumbani humu, kwa sababu huyu naye ni mwana wa Ibrahimu , Luka 19:9.
5. Huduma kwa maskini ni uthibitisho kwa Masihi Yesu wa wokovu wa Mungu ndani ya mtu .
D. Yesu anajihusisha kikamilifu na “walio wadogo” miongoni mwetu, Mt. 25:34-40.
1. Kiti cha Hukumu cha Mfalme, Mt. 25:31-45.
2. Wahusika : seti mbili za watu – kondoo na mbuzi.
4
3. Majibu : mielekeo miwili ya Mfalme, mmoja kwa kondoo, mmoja kwa mbuzi (kundi moja lilibarikiwa na kukumbatiwa, lingine lilihukumiwa na kukataliwa).
4. Hatima mbili : kondoo katika Ufalme walirithi makao ya milele yaliyoandaliwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, mbuzi walirithi moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake.
5. Walengwa ni kundi moja la watu : wenye njaa, wenye kiu, wageni, walio uchi, wagonjwa, wafungwa.
6. Aina mbili tofauti za mwitikio na utendaji : kundi moja lilikuwa na ukarimu na kujali; lingine halikujali wala halikuonyesha upendo.
Made with FlippingBook - Online catalogs