Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 0 6 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

7. Mfalme katika hukumu anatumia kiwango kile kile ili kuamua hatima ya makundi yote mawili: kadiri mlivyomtendea [kwa wema au kwa ubaya] mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo [wanyonge na wahitaji], mlinitendea mimi.

Injili Inawalenga Maskini, Walengwa wa Ufalme

IKatika baadhi ya misemo muhimu sana “maskini” ni wale wanaohubiriwa injili au walengwa wa ufalme. Usemi “maskini wanahubiriwa habari njema” katika jibu la Yesu kwa Yohana Mbatizaji (Mt. 11:5; taz. Lk. 7:22) umeazimwa kutoka katika andiko la Isaya 61:1, ambalo ni andiko la mahubiri ya Yesu ya uzinduzi wa huduma yake huko Nazareti (Lk 4:18). Kule Nazareti andiko hili linatumika kwa kusanyiko dogo katika sinagogi; katika jibu la Yesu kwa Yohana Mbatizaji andiko linahusisha orodha ya miujiza ya Yesu ya uponyaji ambayo inajumuisha maneno yaliyotumika katika Isaya kuzungumzia wokovu wa Israeli. ~ Hans Kvalbein. “Poverty.” The New Dictionary of Biblical Theology. T. D. Alexander, mh. (toleo la Kielektroniki). Downers Grove, IL: IVP, 2001..

8. Utambulisho wa Masihi Yesu na maskini ni kamili, na uhusiano wake na wao unatumika kama msingi na kielelezo cha uhusiano wetu na yeye .

II. Kuonyesha rehema na haki katika jamii ya ufalme

A. Kutangaza Habari Njema kwa maskini

1. Kanisa ni mwili wa Kristo , jamii ya ufalme ya agano jipya iliyoitwa kuendeleza kazi ya Yesu Kristo ulimwenguni kwa njia ya utume na matendo ya haki.

4

a. Washirika wa Kanisa wametiwa muhuri na kupakwa mafuta na Roho yule yule aliyekaa ndani ya Yesu, Efe. 1:13; 4:30; 2 Kor. 1:20-22 pamoja na Luka 4:18-19.

b. Wao ni viungo vya mwili wa Kristo katika ulimwengu, walioitwa kuonyesha tabia ya Ufalme, kwanza katikati yao wenyewe, na kisha kwa ulimwengu .

2. Mitume walimtangaza Yesu kuwa ni Masihi, ambaye ujio wake ulileta uwepo wa wakati ujao, kuanzishwa kwa utimizo wa Ufalme wa Mungu.

3. Yesu wa Nazareti ndiye Masihi wa Mungu, Yohana 1:41-45; Yohana 4:25-26.

Made with FlippingBook - Online catalogs