Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 2 0 7

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

4. Kupitia Yeye, shalom ya haki ya Ufalme wa Mungu ilidhihirishwa kwa kila njia.

a. Matendo 10:36-38

b. Luka 7:21-23

5. Yesu alianzisha jamii ya agano jipya ambayo ameikusudia kuwa onyesho hai la upendo na haki ya Ufalme katika siku hii na saa hii: Kanisa la Yesu Kristo , 1 Kor. 12:27.

6. Kanisa sasa linaishi na kuonyesha maisha ya Enzi Ijayo kupitia matendo mema na utangazaji wa Habari Njema: Utume umeungamanishwa moja kwa moja na matendo yanayoonyesha haki kwa maskini ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa !

4

a. Roho Mtakatifu katika Kanisa ndiye dhamana (arabuni) halisi ya urithi kamili ujao , Efe. 1:13; 4:30; 2 Kor. 1:20-22.

b. Kukusanywa kwa Wayahudi na Wamataifa katika jumuiya moja kwa njia ya imani ni ishara ya shalom itakayokuja juu ya ulimwengu wote wakati wa kukamilishwa kwa Ufalme wa Mungu, Efe. 3:3 10; Rum. 16:24-.; Kol. 1.26-27.

c. Matendo ya haki yanayofanywa ndani ya Kanisa na kupitia Kanisa ni ishara za uwepo wa Ufalme hapa na sasa, Mdo 2 pamoja na Yoeli 2.

7. Kanisa sasa ni Israeli mpya ya Mungu, iliyoitwa kuonyesha viwango na sifa za utawala wa ufalme wa Mungu kwa njia ya mahubiri yake na matendo mema, Gal. 6:16.

Made with FlippingBook - Online catalogs