Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
2 0 8 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
8. Katika jamii hii Wayahudi na Wamataifa wanakusanyika pamoja kama warithi wa ahadi ya Ibrahimu, na warithi pamoja na Kristo.
Ujumbe wa Injili Unawalenga Maskini
a. Gal. 3:14
Ujumbe wa Injili unaonyeshwa vyema katika uhalisia wake miongoni mwa maskini. Katika Injili Yesu alisema kwamba Injili katika utimilifu wake ni maskini na “wenye dhambi.” Mafarisayo waliojiona kuwa wenyehaki wangejifunza asili ya kweli ya Injili ikiwa tu wao pia wangekula pamoja na “wenye dhambi” na kujifunza makundi ambayo yalionyesha vizuri kile ambacho Injili ilimaanisha kwao. Namna pekee ambayo mafarisayo wangebadilishwa na Injili na kuzishuhudia nguvu zake halisi, ni pale tu ambapo na wao pia wangepitia hali ya kutengwa na kukosa msaada kama ilivyokuwa kwa maskini na “wenye dhambi.” ~C. M. N. Sugden. New Dictionary of Theology. S. B. Ferguson, mh. (toleo tepe). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 2000. uk. 524 . “Poverty and Wealth.” The
b. Gal. 3:28-29
9. Sasa, katika maisha na utume wa Kanisa la Yesu Kristo, na kwa nguvu za Roho Mtakatifu, Watu wa Mungu wanaweza kudhihirisha na kufurahia shalom ile ile ya jamii ya agano inayozungumzwa katika Agano la Kale.
a. 1 Pet. 2:9-10
b. Zab. 33:12
4
c. 1 Pet. 1:2
d. 1 Kor. 3:16-17
B. Usawa na rehema: ukarimu unaoshughulikia mahitaji ya msingi ya maisha.
1. Pentekoste : jamii mpya inazaliwa kupitia Neno la Mungu na nguvu za Roho Mtakatifu (Mdo. 2:1-4, 39-39).
2. Upendo na haki ( shalom ) ya jamii ya agano la Mungu vinaonyeshwa katika siku ya kwanza ya kuundwa kwa jamii hiyo, Mdo 2:42-47.
Made with FlippingBook - Online catalogs