Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 0 9
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
3. Mwendelezo wa ujazo na kutiwa nguvu na Roho Mtakatifu unaonyesha haki, utakatifu, na umoja wa watu wa agano wa Mungu.
a. Matendo 4:31-35
b. Kanisa linaonyesha shalom ya jamii ya agano ya Mungu, Kumb. 15:4-6; taz. Kumb. 2:7; Zab. 34:9.
4. Kanisa linaweka mikakati ya kukidhi mahitaji ya wajane na maskini walio katikati yake, taz. Mdo 6:1-6 pamoja na 1 Timotheo 5.
a. Matendo makubwa ya ukarimu, Mdo 4:35.
b. Rejesta rasmi ziliwekwa ili kukidhi mahitaji ya wale ambao walikuwa maskini na wasio na vitu, 1 Tim. 5:9.
4
5. Ugawaji wa mali : makanisa yote ya Makedonia na kwingineko yalifanya changizo ili kusaidia kanisa la Yerusalemu wakati wa njaa, Mdo. 11:27-30, taz. 2 Kor. 8-9.
C. Utetezi kwa ajili ya maskini: alama mahususi ya utume halisi wa Kikristo.
1. Kutokuwa na upendeleo wala utofauti katika namna ya kuwatendea maskini na matajiri, Yak. 2:1-7; 5.1-4.
a. Mungu amewafanya maskini kuwa matajiri katika imani na warithi wa Ufalme wa Mungu (Yak 2:5).
Made with FlippingBook - Online catalogs