Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
2 2 0 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
³ Kanisa lazima litende kwa kuzingatia kwamba Mungu amewachagua maskini. Hilo linamaanisha kwamba lazima Kanisa litetee maslahi yao, lidumishe haki zao, na kutoonyesha upendeleo katika mambo yetu katika Kanisa. Tunapaswa kuwa wakarimu katika kukidhi mahitaji ya maskini, kugawana mali zetu, kuwafadhili wageni na wafungwa, na kuonyesha upendo kama tulivyoonyeshwa. ³ Katika utoaji wetu wote na kujali kwetu, tunapaswa kutafuta haki na usawa kwa maskini, popote tunapowapata. Hatutakiwi kukidhi mahitaji yao kijuujuu tu, bali kujitahidi kushughulika na mifumo na mahusiano kwa namna ambayo itachochea hali ya haki zaidi, yaani kuishi “Injili ya mafanikio” ya kweli, ambayo ni kutafuta haki na usawa kwa niaba ya walio hatarini zaidi miongoni mwetu. Sasa ni wakati wa wewe kujadili na wanafunzi wenzako maswali yako kuhusu utume wa Kikristo na maskini. Maswali yafuatayo yanalenga kuibua maswali yako mwenyewe kuhusu maoni yako binafsi na imani yako kuhusiana na maskini, na uhusiano wako nao. Tengeneza maswali yako mwenyewe unapotafakari na uwashirikishe wanafunzi wenzako yale utakayoyapata kupitia kutafakari kwako. * Unaelewa nini sasa kuhusu shalom , baada ya kupata utangulizi huu wa dhana hihi? Kwa nini dhana hii inaweza kuwa muhimu kwa maisha yako mwenyewe na huduma mahali unapoishi na kumtumikia Bwana hivi sasa? * Ni kwa njia gani umeishuhudia shalom katikati ya familia yako na kanisa lako la mahali pamoja tangu ulipomkubali Kristo (yaani, fikiria kwa kuzingatia sifa kuu za shalom : uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu). * Je, umekua katika umaskini, au unamjua mtu fulani ambaye alikua katika umaskini? Je, hali hiyo imeathiri namna gani uelewa wako kuhusu maisha ya Kikristo leo? * Kwa nini tunaweza kusema kwamba umaskini ni kunyimwa shalom ya Mungu? Ikiwa ulikua katika hali ya umaskini, ulishuhudiaje ukweli huu, kibinafsi? Eleza. * Kati ya sababu tatu za umaskini zilizotajwa katika Maandiko (yaani, maafa na majanga ya asili, uvivu wa kibinafsi na uzembe, na ukandamizaji na dhuluma kutoka kwa wenye nguvu) unadhani ni sababu ipi ambayo huleta fedhea zaidi kwa maskini? Je, unadhani ni sababu ipi kati ya hizo ambayo
Kutendea Kazi Somo na Matokeo yake kwa Wanafunzi
4
Made with FlippingBook - Online catalogs