Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
/ 2 2 1
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
Kanisa linaelekea kuishughulikia zaidi? Ni sababu ipi haizingatiwi wala kushughulikiwa sana? * Kamilisha usemi ufuatao: “Ikiwa ningetakiwa kueleza mtazamo wangu wa sasa kuhusu maskini kwa neno moja au katika sentensi moja ningesema. . . * Je, wewe binafsi umehusika vipi katika huduma zinazohudumia maskini? Je, ulikuwa na mitazamo gani ulipokutana na kushughulika nao? Je, umeona ugumu wowote kuwapenda na kuwatumikia maskini? Elezea jibu lako? * Je, kwa sasa unashiriki katika huduma pamoja na mtu mmoja wa kundi la Yesu la “hao ndugu zangu walio wadogo” (yaani, wenye njaa, wenye kiu, wageni, walio uchi, wagonjwa, na wafungwa)? Je, ni aina gani za mitazamo na uelewa unaohitajika ili kuhudumu kwa ufanisi miongoni mwao? * Je, wale wanaokujua wangekutambulisha kuwa mkarimu na mkaribishaji wageni? Unafikiri ni kwa nini sifa hizi zimepewa nafasi kubwa kuhusiana na maadili ya Ufalme katika Agano Jipya? * Ikiwa mtu ni bahili na mbinafsi, ni njia gani bora zaidi ya yeye kujifunza jinsi ya kuwa mkarimu na mkaribishaji-wageni? Kwa nini ni muhimu kuwatafuta wajane, yatima, na maskini ili kuwahudumia, hata kama kuwatafuta ni vigumu na ni jambo ambalo hatujalizoea? * Je, unadhani ni rahisi kuamini katika mabadiliko ya watu maskini – ni aina gani ya mtazamo ambao kwa kawaida unauonyesha kwa wengine kuhusu watu ambao ni maskini? Je, umezoea kuwalaumu maskini kwa matatizo yao, au una mwelekeo wa kuwaheshimu kama watu waliochaguliwa na Mungu? * Malizia sentensi ifuatayo: “Ikiwa Mungu angefanya jambo moja tu katika mtazamo na maisha yangu ili kunifanya niwe mwenye matokeo zaidi katika kuwatunza watu ambao wako katika umaskini, ningemwomba . . .
4
Made with FlippingBook - Online catalogs