Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi
2 2 2 /
MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO
MIFANO
Tatizo la Katrina
Marekani nzima ilitazama kwa hofu wakati kimbunga Katrina kilipopiga jiji kuu la kusini la New Orleans, na kuathiri maelfu ya maskini wa mijini ambao walikuwa wamekwama bila chakula, maji, wala misaada. Kuwaona wazee, vijana, na watu wengi wenye uhitaji wakiteseka vibaya katika hali duni ya maisha lilikuwa jambo lililoleta uchungu mwingi; hakuna visingizio vyovyote, kulaumiana, au maelezo kuhusu ahadi za “wakati ujao” ambayo yangeweza kuleta utulivu au faraja kwa wengi ambao bado, hadi leo hii, wanateseka bila kazi, msaada wa kifedha, au wazo lolote kuhusu hatua zinazofuata maishani mwao. Sababu nyingi zimetolewa kuhusu ukosefu wa huduma kwa watu wale maskini: «Watu wale walikuwa maskini na weusi, na kundi hili la watu halijawahi kuchukuliwa maanani sana katika historia ya Marekani,» «Watu wale hawakutii wito wa kuondoka jijini wakati walikuwa na nafasi hiyo,» «Mashirika ya kiserikali yalizembea kushughulikia shida ile kabla haijafika na ilipofika, hayakuwa na uwezo wa kukabiliana na matokeo yake» – sababu hizi na zingine zimetolewa ili kujaribu kuelezea maafa mengi ya asili yaliyoathiri maisha ya watu wengi. Katika kufikiria juu ya uwezekano wa maafa na majanga ya asili, nini maoni yako kuhusu nani anayehusika na huduma wakati na baada ya matukio haya: watu wenyewe, mashirika na mamlaka za kiserikali, Kanisa na mashirika mengine ya misaada, au wote hao, kuungana pamoja kwa nama moja au nyingine? Theolojia ya ukombozi bila shaka ndiyo maendeleo muhimu zaidi ya kitheolojia katika karne ya 20. Aina mbalimbali za theolojia ya ukombozi huzingatia dhamira kuu ya Mungu wa Maandiko kuwa ni Mungu wa maskini na waliokandamizwa. Nyenzo zote za kibiblia na taaluma za kitheolojia hupimwa kwa kuzingatia jinsi zinavyofafanua utambulisho huu wa msingi wa Mungu na maskini, waliotengwa, wanyonge, wasio na uwezo, na wahitaji. Katika kanisa fulani, kiongozi mmojawapo mwenye nafasi muhimu na pia ni mwalimu wa Neno, ameathiriwa sana na usomaji wake wa vitabu kadhaa vya theolojia ya ukombozi vinavyohusu dhana ya umaskini. Anaamini kwamba ingawa baadhi ya mambo yanayozungumzwa katika vitabu hivyo hayana msingi wa kibiblia wala hayamo kabisa katika Maandiko, kuna sehemu zinazotoa ufahamu wa kina kuhusu hali ya uonevu, umaskini, na maisha katika majiji. Kiongozi huyo anasema kwamba kanisa lao anakoabudu ambalo ni la mjini na linatunza familia zilizokumbwa na uraibu, dawa za kulevya, au unyanyasaji, lingeweza kutumia baadhi ya maarifa na maneno ya kutia moyo yaliyomo katika vitabu hivyo. Anaamua kuleta baadhi ya maarifa hayo katika darasa lake la watu wazima wa Umri wa Chuo, si kwa lengo la kuleta mabishano bali kunyoosha Theolojia ya Ukombozi na Dhana ya Umaskini
1
4
2
Made with FlippingBook - Online catalogs