Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

/ 2 2 3

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

akili za wanafunzi ili waweze kumfikiria Mungu zaidi katika maana ya historia ya kitabu cha Kutoka—Mungu mkombozi wa maskini. Baadhi ya walimu wengine wana wasiwasi juu ya athari ya elimu hiyo kwenye akili za wanafunzi, hasa wale ambao bado ni wachanga katika imani na ambao wanaweza kukengeuka kirahisi kwa kushindwa kupambanua mafundisho hayo. Kama ungekuwa mchungaji wa kanisa kama hilo, ungeshughulikiaje hali hii? Kwa kuzingatia nia ya dhati ya mwalimu huyu ya kufundisha wanafunzi kuhusu moyo wa Mungu kwa maskini, ni utaratibu gani au njia gani mbadala ungeipendekeza kwake ili apate kuitumia? (Inatokana na kisa cha kweli). Dada mpendwa (tutamwita Sharon) ambaye aliokolewa kutoka katika maisha ya zamani yenye matatizo ya uraibu wa dawa za kulevya na pombe alikuwa amejiunga na ushirika wa kanisa hivi majuzi. Ni dada aliyeokoka kweli kweli, na mwenye shauku kubwa ya kukua katika Kristo, lakini bado alikuwa Mkristo mchanga. Mahusiano mengi aliyokuwa nayo katika maisha yake ya zamani kimsingi yalikuwa mahusiano na watu waliompa Sharon msaada kutoka katika shida moja na nyingine. Kwa namna fulani, dada yule aliendelea kuhusiana na watu kwa njia hii, na kutokana na shauku yake ya mabadiliko, wengi waliona mahusiano ya aina hii kuwa sahihi. Mambo yalibadilika pale dada huyu alipoanza kuja kanisani akiwa ametumia madawa ya kulevya na mlevi, na wengi hawakusema wala hawakufanya lolote kuhusu hilo. Sharon alipendwa sana, alithaminiwa na wote, na kila mtu alikuwa akimtetea kwa imani kwamba atabadilika. Hakuna aliyetaka kumhukumu au kumvunja moyo sana kwa hofu kwamba angeshawishika kurudia maisha yake ya uasherati. Mchungaji wa kanisa hilo, ambaye kama kila mtu mwingine alimjali Sharon lakini pia alitaka kumwona akiwa amekomaa katika Kristo, alitaja hali ya kuja kanisani akiwa amelewa kuwa jambo lisilokubalika kama Mkristo. Kwa kuwa sasa yeye ni wa Kristo, ni lazima ajitie nidhamu ndani yake ili kujiepusha na mambo ya aina hii, na ikibidi, achukue hatua zaidi ili kupata msaada anaohitaji, hata ikiwezekana hatua ya kuingia katika mpango wa matibabu ya dawa za kulevya na vileo. Aliposikia ushauri huu, dada huyo mpendwa aliudhika, na kuzungumza na washirika kadhaa kuhusu ukosefu wa ufahamu na subira ambao mchungaji alikuwa ameonyesha. Washirika wengine walimkabili mchungaji, wakimkumbusha juu ya hitaji la subira na upendo na asiwe mtu mkali na wa kuhukumu wengine. Kutokana na maelezo ya kisa hiki, ungekuwa na ushauri gani kwa kanisa hili wanapojaribu kutafuta namna bora ya kumtunza Sharon? Kati ya mitazamo hii miwili (mtazamo wa Mchungaji na ule wa washirika wanaopinga mtazamo wa Mchungaji), ni mtazamo wa nani ni wenye huruma, na mtazamo wa nani unaelekea kwenye uraibu wa utegemezi? 3 Uraibu wa Utegemezi au Huruma?

4

Made with FlippingBook - Online catalogs