Misingi ya Utume wa Kikristo, Mwongozo wa Mkufunzi

2 2 4 /

MISINGI YA UTUME WA KIKRISTO

Matangazo Kupitia Maskini

Mojawapo ya mazoea ya kawaida leo kwa mashirika ya kutoa misaada na huduma zinazoshughulikia mahitaji ya watu maskini ni kuonyesha picha zenye kuhuzunisha za hali mbaya ya mazingira wanayoishi kwa ajili ya kuhamasisha watu kutoa. Zoezi hili limekuwa jambo la kawaida katika maeneo mengi; ushuhuda wa maskini hutumika kama njia ya kukusanya fedha kwa ajili ya kazi halali ya utoaji misaada, uwezeshaji, na huduma za dharura. Tatizo la mbinu za aina hii ni jinsi watu maskini wanavyoonekana. Labda bila kuzingatia kwa umakini, mazoea kama haya yanaweza kusababisha kwa urahisi kuimarisha dhana fulani juu ya maskini ambayo si lazima iwe kweli. Maskini wengi nchini Marekani, kwa mfano, ni weupe, si Weusi wala wa asili ya Asia, na wengi wao wana kazi. Picha za watu masikini zinazozunguka kila mahali ni zile za mwanamke mweusi maskini au mtoto mweusi mwenye utapia mlo, na hizi zimeenea kila kona kiasi kwamba imekuwa kawaida na jambo linalokubalika. Shirika moja la kimisheni, katika jaribio la kubadilisha aina hizi za mazoea, lilibadilisha mfumo wake wa kutangaza kazi zake. Badala ya kuangazia hali mbaya zaidi za familia zenye uhitaji zaidi katika hali zao duni zaidi, shirika hili liliamua kuzungumza juu ya njia ambazo Bwana alikuwa akibadilisha maisha ya watu maskini. Mtazamo haungekuwa tena juu ya hali ya zamani ya watu, bali walizungumza zaidi kuhusu matumaini ya siku zijazo za watu waliowahudumia. Wengine katika shirika hilo hawana uhakika kwamba mbinu hii mpya itasaidia. Wanasema kwamba picha za maisha halisi ya watu maskini zilizomo katika vipeperushi, tovuti na mitandao yao ni za ukweli mtupu; ni suala la kuwa wazi juu ya kile hasa kinachoendelea. Zaidi ya hayo, wanasema kwamba ikiwa watu hawataona mahitaji halisi na kushawishiwa kuhusu njia za kusaidia, hawatajali sana kuhusu «hadithi za mafanikio» tunazotoa. Watakuwa na furaha kwa ajili yetu na kazi zetu, lakini hawatatusaidia kifedha. Je, ungelishauri nini shirika hili la kimisheni kama wangeuliza maoni yako kuhusu jinsi wanavyopaswa kuelezea kazi zao za kusaida maskini? Je, kuna njia ya kuwasilisha mahitaji ya watu bila kuanika picha za watu maskini kwa namna inayoshusha heshima yao, na kuwalazimisha kutweza utu wao kutokana na njia tunazotumia kukusanya rasilimali za kuwasaidia? Dhana ya maskini imejengwa juu ya maono ya kibiblia ya shalom, au ukamilifu: shalom ni neno la Kiebrania linalomaanisha «ukamilifu wa jamii ya wanadamu katika ushirika na Mungu na baina yao mmoja kwa mwingine.» Vipengele vya kibiblia vya shalom ni pamoja na uzima na afya njema, usalama na ulinzi, maelewano kati ya majirani, ustawi na utoshelevu wa mali, na kukosekana kwa uovu na migogoro – Amani ya kweli na kamilifu. Hili pia linajumuisha wazo la shalom kama utoaji wa Mungu kwa msingi wa neema yake, unaohusishwa na ujio wa Masihi ambaye

4

4

Marudio ya Tasnifu ya Somo

Made with FlippingBook - Online catalogs