Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 2 | KUTAF S I R I B I B L I A : MB I NU YA HATUA TATU / 109
1. “ Kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza : Hatua ya kwanza inalenga kuelewa maandiko yalimaanisha nini katika muktadha wake wa asili.”
2. Ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno : Hatua ya pili inalenga kupata kanuni za kibiblia katika maandiko hayo ambazo zinawahusu waamini leo.
3. Ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu : hatua ya tatu ni kuhusianisha kanuni za Kweli ya Neno na maisha yetu binafsi katika nguvu za Roho Mtakatifu.
B. Dhumuni
1. Kujifunza mwandishi alimaanisha nini katika muktadha wa kwanza wa andiko.
2
M A S O M O Y A B I B L I A
2. Kutambua kanuni za kibiblia zinazotoa muhtasari wa maandiko na kutoa hekima ya Mungu na ufahamu ambao unawahusu watu wote na unaweza kutumika kwa wote.
3. Kubadili mitazamo na matendo yetu na kuyafanya maisha yetu yaendane na kweli zilizomo katika Neno la Mungu.
C. Vipengele.
1. Inawiana na mbinu ya sarufi ya kihistoria : kutafuta maana ya maandiko katika mazingira yake ya asili kabla ya kutumia maana yake katika zama na mazingira tofauti.
2. Mbinu hii inatafuta maana ya wazi (dhahiri, isiyofichika) ya maandiko.
3. Mbinu hii inathibitisha ufunuo endelevu .
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker