Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

110 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

a. Biblia inaonyesha kwamba Mungu ameendelea kufunua maana na njia ya kusudi lake, ambalo lina kilele chake (yaani, “linahitimishwa”) katika Yesu Kristo, Ebr. 1:1-3.

b. Yesu yuko juu ya yote na anatimiza maana ya yote ambayo Mungu ameyasema tangu mwanzo (taz 1:14 18; Mt. 5:17-18; Yoh 5:39-40; Lk 24:27, 44-48).

4. Inathibitisha umoja wa maandiko .

a. Biblia ni kanoni moja (mkusanyiko, maktaba) ya maandiko, iliyoandikwa na mwandishi mmoja (2 Tim. 3:16-17; 2 Pet. 1:20-21).

b. Mada ya wazi ya maandiko ni Yesu Kristo na Ufalme wake, Mdo 28:23,31; Kol. 1:25-27; Efe. 3.3-11; Rum. 16.25-27.

2

M A S O M O Y A B I B L I A

5. Mbinu hii inathibitisha ukweli wa andiko : waandishi wakiongozwa na Roho Mtakatifu waliwasilisha mtazamo na ukweli ambao Mungu aliukusudia kwa wasikilizaji wa kwanza, ambao tunaweza kuugundua na kuuishi (1 Kor. 10:1-6).

D. Faida zake

1. Ni mbinu ya kuyaendea maandiko kwa madhumuni ya ufafanuzi ( exegesis ).

2. Njia hii inasisitiza kuelewa kabla ya kufanyia kazi.

3. Kutafuta kanuni za nyakati zote [za milele] katika maelezo na matukio yahusuyo wakati fulani mahususi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker