Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
140 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I
Kutolewa kwa Ahadi Ahadi na Utimilifu katika Agano la Kale na Agano Jipya
Mch. Dkt. Don L. Davis
MAUDHUI
Uhusiano wa Agano la Kale na Agano Jipya unaweza kueleweka vyema kupitia wazo la ufunuo endelevu , ambao unathibitisha kwamba Mungu amejifunua hatua kwa hatua na kwa uhakika katika historia ya watu wake, na hatimaye kupitia Yesu Kristo. Mungu kwa namna mbalimbali na nyakati tofauti-tofauti alijidhihirisha kwa taifa la Israeli kwa kiwango fulani, lakini katika siku hizi za mwisho amesema nasi wazi wazi kwa njia ya Mwanaye. Yesu wa Nazareti ndiye ufunuo wa mwisho na kamili wa Mungu juu yake mwenyewe, ambao sasa unashuhudiwa katika Maandiko. Kama asemavyo Agustino: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Uhusiano wa AK na AJ uhusiano kamilishi, Agano la Kale likitoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, Agano la Kale linasimama kama matarajio ya kilele cha Agano Jipya kuhusu hadithi ya wokovu wa Mungu katika Kristo. Zaidi ya hayo, Agano la Kale linaonyesha utu wa Kristo na kazi yake iliyojumuishwa kikamilifu katika Agano Jipya. Ingawa Agano la Kale ni ufunuo wa awali na hafifu wa wokovu wa Mungu, Agano Jipya linaweza kuonekana kama la mwisho lililokamilishwa, na wito wa ulimwengu wote ambao katika Agano la Kale umeainishwa kimahususi kwa taifa la Israeli. Muunganiko wa maagano haya unaweza kuonekana katika ahadi na mada ya utimilifu, hasa kwa namna Agano Jipya linavyothibitisha kwamba kazi ya Agano la Kale ni kutoa ushuhuda wenye nguvu na wa uhakika kuhusu Masihi, kupitia historia ya mababa wa imani, Taifa la Israeli, unabii mbalimbali juu ya Masihi, na viwango vya maadili vya Sheria. Ushuhuda huo umetimizwa katika Yesu Kristo. Lengo letu la somo hili, Ahadi na Utimilifu katika Agano la Kale na Agano Jipya , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Uhusiano wa Agano la Kale na Agano Jipya unaweza kueleweka kwa ufanisi kupitia wazo la ufunuo endelevu , ambao unathibitisha kwamba Mungu amejifunua hatua kwa hatua na kwa uhakika katika historia yote ya watu wake, na hatimaye kupitia Yesu Kristo. • Dhana ya ufunuo endelevu ni pamoja na ufunuo endelevu wa Mungu kwetu kupitia uumbaji, kupitia madhihirisho na matukio maalum, na katika siku hizi za mwisho kupitia Mwanawe. Agano la Kale linalielezea na kulifunua Agano Jipya kupitia Kristo, na maagano yote mawili yanalenga ufunuo wa mwisho na kamili wa Mungu juu yake mwenyewe katika Yesu Kristo na utawala wa ufalme wake.
Muhtasari
3
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker