Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 141

• Epigramu (msemo) ya Agustino inafupisha vizuri uhusiano kati ya maagano haya mawili: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Uhusiano huu kamilishi unaonekana katika jinsi Agano la Kale linavyotoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, matarajio ya Agano la Kale juu ya Masihi na kazi yake, na utambulisho katika Agano Jipya wa Yesu wa Nazareti kama kilele cha matarajio hayo. Pia, Agano la Kale linatumika kama kivuli (kielelezo) cha Kristo na kazi yake na Agano Jipya kama utimilifu wake, na Agano la Kale linaonekana kama ufunuo wa awali na hafifu wa wokovu wa Mungu uliokamilishwa baadaye katika ufunuo wa Yesu katika Agano Jipya. Hatimaye, kile ambacho kiliwekwa maalum kwa Israeli katika Agano la Kale kilienezwa kwa mataifa yote katika Agano Jipya. • Mada ya ahadi na utimilifu katika ufunuo wa Agano la Kale inathibitisha ahadi ya Mungu kwa mteule wake mwenyewe kuwakomboa wanadamu na kuharibu kazi ya shetani, ahadi iliyotimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. • Agano Jipya linatoa vifungu kadhaa vya msingi ambavyo vinathibitisha kwamba kazi ya Agano la Kale ilikuwa ni kutoa ushuhuda wenye nguvu na wa uhakika kwa habari ya Masihi uliotimizwa katika nafsi ya Yesu Kristo (taz. Lk 22:25-27, 44 48; Mt. 5:17-18; ; Yoh 1:45; 5:39-40; Ushahidi huo unaweza kuonekana katika historia ya mababa wa kale wa imani, Taifa la Israeli, unabii mbalimbali wa Kimasihi, na viwango vya maadili vya Sheria.

3

M A S O M O Y A B I B L I A

I. Ufunuo endelevu : Kuthibitisha Muunganiko Kati ya Agano la Kale na Agano Jipya

Muhtasari wa Maudhui ya Video

A. Maana ya ufunuo endelevu : Mungu amejidhihirisha hatua kwa hatua kupitia historia na hatimaye kupitia Yesu Kristo. Ebr. 1:1-2 - Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, 2 mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana, aliyemweka kuwa mrithi wa yote, tena kwa yeye aliufanya ulimwengu.

Epigramu ya Agustino kuhusu uhusiano kati ya maagano mawili: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.”

B. Vipengele vya ufunuo endelevu

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker