Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 143

f. Anatimiza maneno ya Agano la Kale, pamoja na unabii wa Torati na Manabii, Lk 24:25-27.

g. Anamfunua Mungu kupitia nafsi yake mwenyewe (yaani, yeye ni mfano dhahiri wa utukufu wake, “Neno aliyefanyika mwili,” taz. Yoh. 1:14-18).

5. Agano la Kale linaeleza na kufunua maana ya Agano Jipya.

C. Matokeo ya ufunuo endelevu katika ufasiri wa Maandiko katika msingi wa Kristo

1. Kuna muunganiko wa karibu kati ya Agano la Kale na Agano Jipya.

2. Maagano yote yanalenga ufunuo wa Mungu kuhusu Yesu Kristo na utawala wa ufalme wake.

3

II. Dhana Kamilishi Zinazounganisha Agano la Kale na Agano Jipya Epigramu (msemo mdogo) ya Agustino kuhusu uhusiano kati ya maagano mawili: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” A. Utangulizi na hitimisho : Agano la Kale linatupatia utangulizi wa kweli kuhusu Kristo na Ufalme wake, na Agano Jipya linayaleta haya kwenye hitimisho (k.m., mafundisho ya Mtumishi katika Isaya sura ya 42-55 yanamtambulisha mtu ambaye kwa hakika anaonekana kuwa ni Yesu Kristo katika ujio wake wa kwanza [rej. 1 Pet. 1:22-25]). B. Matarajio na kilele : kile kinachotarajiwa kuhusu Kristo na Ufalme wake katika Agano la Kale kinaletwa kwenye kilele chake cha mwisho katika Agano Jipya (wokovu wa mabaki ya Israeli katika Zek. 12:10-13:1 ni taraja la kilele cha kurudi kwa Yesu Ufunuo 19).

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker