Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

144 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

C. Kivuli na Utimilifu : kile ambacho kimetambulishwa na kuonyeshwa kwa njia ya kivuli katika Agano la Kale kuhusu Kristo na Ufalme wake kimefunuliwa na kupata utimilifu wake katika Agano Jipya (hema ya kimwili ya Waebrania 8:5 ni kivuli cha hema ya kweli inayotajwa kuhusu Yesu kama kuhani mbinguni). D. Udhaifu wa AK na Ukamilifu wa AJ : kile kinachoonyeshwa na kuonekana kuwa dhaifu au hafifu katika Agano la Kale kimekamilishwa na kuhitimishwa katika Agano Jipya (k.m., kitabu kizima cha Waebrania kinazungumza juu ya kutotosheleza kwa mfumo wa dhabihu wa kale katika kuondoa dhambi; Kifo cha Yesu ni uhalisia wa ufanisi ulio nyuma ya kivuli cha Agano la Kale, k.m., Ebr. 10:1-10).

E. Suala mahususi na baadaye la mataifa yote : kile ambacho ni maalum kwa watu wa Israeli katika Agano la Kale kinapanuliwa na kuenea kwa wote wanaoamini katika Agano Jipya.

III. Ahadi na Utimilifu: Kristo kama Msingi wa Ufunuo wa Agano la Kale

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Kristo Ndiye Mada ya Kila Moja ya Sehemu Nane za Biblia (Ona Geisler, A Popular Survey of the Old Testament , uk. 21-24) 1. Sheria (Mwanzo - Kumbukumbu la Torati): Kuweka Msingi kwa ajili ya Masihi 2. Historia (Yoshua - Esta): Maandalizi kwa ajili ya Masihi 3. Ushairi (Ayubu - Wimbo Ulio Bora): Matarajio ya Masihi 4. Unabii (Isaya - Malaki): Matarajio ya Masihi 5. Injili (Mathayo - Yohana): Udhihirisho wa Masihi 6. Historia (Matendo): Kuenezwa kwa habari njema za Masihi 7. Nyaraka (Warumi - Yuda): Tafsiri na Matumizi ya Ujumbe wa Masihi 8. Unabii (Ufunuo): Utimilifu wa Mambo Yote katika Masihi.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker