Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 145
A. Ufafanuzi wa mada ya utimilifu wa ahadi : ahadi ya Mungu kwamba mtu mmoja angewakomboa wanadamu kutoka katika dhambi zao na kuharibu kazi ya shetani inatimizwa katika Yesu Kristo.
B. Yesu anatoa ushuhuda wenye kushawishi ndani ya Maandiko kwamba kusudi la Agano la Kale ni kutoa ushuhuda kuhusu Yeye na kazi yake.
1. Barabara ya kwenda Emau
a. Luka 24:25-27, 32
b. Hapa kuna picha ya Kristo akifasiri Maandiko yote (yaani, Agano la Kale) jinsi yanavyoeleza na kuelekeza kwenye utambulisho wake mwenyewe.
2. Kuonekana kwake baada ya ufufuo
3
a. Luka 24:44-48
M A S O M O Y A B I B L I A
b. Kristo alifungua akili zao wapate kuyaelewa Maandiko (yaani, Agano la Kale) kumhusu yeye mwenyewe.
3. Hotuba ya Mlimani
a. Mt. 5:17-18
b. Mafundisho ya Kristo ya wazi kwamba hakuja kutangua Maandiko bali kuyatimiliza.
4. Mazungumzo na Mafarisayo
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker