Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

146 / MTAALA WA CORNERS TONE K I TABU CHA MWANAFUNZ I

a. Yoh. 5:39-40

b. Yesu akiwaeleza wataalamu wa Maandiko kwamba kuyasoma bila kuzingatia utambulisho wake ni ufafanuzi mbaya na usiofaa wa Maandiko.

5. Nukuu ya kinabii katika Ebr. 10:5-10 taz. Zab. 40:6-8

a. Zab. 40:6-8

b. Ebr. 10:5-10

c. Zaburi hii ya kinabii inahusishwa na Yesu Kristo anapohusisha kifungu hicho na sadaka ya mwili wake mwenyewe kama dhabihu ya dhambi.

C. Athari za mada ya utimilifu wa ahadi Luka 24:44-48 - Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. 45 Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. 46 Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; 47 na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. 48 Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya..

3

M A S O M O Y A B I B L I A

1. Katika historia ya Mababa, taifa la Israeli, na maendeleo yake ya kihistoria na kiroho, Agano la Kale linatupatia picha ya wazi ya Kristo.

2. Ahadi kuu ya Mungu katika Agano la Kale (yaani, kwamba Mungu angetuma Mzao/Mtumishi ambaye angerekebisha anguko la uumbaji wake na wanadamu wote) inatimizwa katika udhihirisho wa Yesu Kristo uliorekodiwa katika Agano Jipya.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker