Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi
SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 147
3. Mada halisi ya Maandiko ni moja na yenye nguvu: ufunuo wa Yesu Kristo.
4. Agano la Kale linaweza kusomwa kwa faida kama muhtasari wa ahadi ya Mungu ya wokovu na urejesho wa ufalme ambao Agano Jipya ni utimilifu wake.
Hitimisho • Dhana ya ufunuo endelevu inaunganisha uelewa wetu wa Agano la Kale na Agano Jipya katika nafsi ya Yesu Kristo na utawala wa ufalme wake. • Agano la Kale na Agano Jipya zinakamilishana, na kupitia mada ya kibiblia ya ahadi na utimilifu tunaweza kufahamu maana na matumizi ya Agano la Kale. Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine ambayo yameibuka kutokana na video. Katika somo hili tumeangazia uhusiano wa Agano la Kale na Agano Jipya katika dhana ya ufunuo endelevu , pamoja na mada ya ahadi na utimilifu . Wazo la ufunuo endelevu linathibitisha kwamba Mungu amejifunua hatua kwa hatua na kwa uhakika katika historia yote ya watu wake, na hatimaye kupitia Yesu Kristo. Vivyo hivyo, dhana ya ahadi na utimilifu wake inamaanisha kwamba ahadi ya Mungu ya kukomboa na kurejesha uumbaji na watu wake, iliyofanywa katika Agano la Kale, inatimizwa kupitia Yesu wa Nazareti katika Agano Jipya. Chunguza mawazo haya na mengine yaliyotolewa katika somo hili kwa kurejea maudhui ya somo kupitia maswali yaliyo hapa chini. Tumia Maandiko katika majibu yako, pale inapofaa. 1. Ufunu endelevu maana yake nini, na wazo hilo linathibitisha nini kuhusu Mungu na azimio lake la kujitangaza mwenyewe ulimwenguni? Toa jibu mahususi na la uhakika. 2. Je, dhana ya ufunuo endelevu inatusaidiaje kuelewa jinsi ambavyo Mungu amejifunua kwa wanadamu kabla ya Kristo? Sasa kwa kuwa Kristo amekuja, ni ufunuo gani zaidi tunaoweza kutarajia kutoka kwa Mungu kuhusu yeye mwenyewe na makusudi yake kwa ulimwengu wake wote? 3. Ni usemi gani wa Agustino unaofupisha vizuri uhusiano kati ya maagano mawili? Eleza maana yake. 4. Je! ni baadhi ya njia zipi ambazo Agano la Kale na Agano Jipya yanakamilishana, yaani, AK kulielezea AJ huku AJ
Maswali kwa Wanafunzi na Majibu Ukurasa wa 87 5
3
M A S O M O Y A B I B L I A
Made with FlippingBook Digital Proposal Maker