Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 149

ufunuo wa mwisho na kamili wa Mungu juu yake mwenyewe katika Yesu Kristo na utawala wa ufalme wake. • Epigramu (msemo) ya Agustino inafupisha vizuri uhusiano kati ya maagano haya mawili: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Uhusiano huu kamilishi unaonekana katika jinsi Agano la Kale linavyotoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, matarajio ya Agano la Kale juu ya Masihi na kazi yake, na utambulisho katika Agano Jipya wa Yesu wa Nazareti kama kilele cha matarajio hayo. Pia, Agano la Kale linatumika kama kivuli (kielelezo) cha Kristo na kazi yake na Agano Jipya kama utimilifu wake, na Agano la Kale linaonekana kama ufunuo wa awali na hafifu wa wokovu wa Mungu uliokamilishwa baadaye katika ufunuo wa Yesu katika Agano Jipya. Hatimaye, kile ambacho kiliwekwa maalum kwa Israeli katika Agano la Kale kilienezwa kwa mataifa yote katika Agano Jipya. • Mada ya ahadi na utimilifu katika ufunuo wa Agano la Kale inathibitisha ahadi ya Mungu kwa mteule wake mwenyewe kuwakomboa wanadamu na kuharibu kazi ya shetani, ahadi iliyotimizwa katika nafsi ya Yesu wa Nazareti. • Agano Jipya linatoa vifungu kadhaa vya msingi ambavyo vinathibitisha kwamba kazi ya Agano la Kale ilikuwa ni kutoa ushuhuda wenye nguvu na wa uhakika kwa habari ya Masihi uliotimizwa katika nafsi ya Yesu Kristo (taz. Lk 22:25-27, 44 48; Mt. 5:17-18; ; Yoh 1:45; 5:39-40; Ushahidi huo unaweza kuonekana katika historia ya mababa wa kale wa imani, Taifa la Israeli, unabii mbalimbali wa Kimasihi, na viwango vya maadili vya Sheria. • Mada kuu inayounganisha ufunuo wote wa Biblia katika Maandiko ni mada ya ahadi na utimilifu . Mada hii inathibitisha umoja wa Agano la Kale na Agano Jipya, katika suala la dhamira ya Mungu kujidhihirisha mwenyewe, kuwakomboa watu wake, na kufanya hivyo kupitia ahadi iliyotolewa kwa Ibrahimu na uzao wake ambayo ilitimizwa katika Yesu wa Nazareti.

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Namuona MolaWangu Kitabuni Ninampata Bwana wangu katika Biblia, popote niangaliapo, Yeye ndiye mada ya Biblia, kiini na moyo wa Kitabu; Yeye ni Ua la Sharoni, Yeye ndie urembo wa Yungiyungi, Popote ninapofungua Biblia yangu, Bwana wa Kitabu yuko hapo.

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker