Mtaala wa Cornerstone, Kitabu cha Mwanafunzi

SOMO LA 3 | USHAHIDI WA AGANO LA KALE KUHUSU KRISTO NA UFALME WAKE: KUTOLEWA KWA AHADI / 151

gani ufahamu wangu wa kanuni hii uliathiri jinsi nilivyosoma na kutumia Agano la Kale na Agano Jipya? • Je, nina mwelekeo wa kusisitiza uhusiano na mwendelezo uliopo kati ya Agano la Kale na Agano Jipya, au ninasisitiza zaidi tofauti kati ya maagano hayo? Elezea. • Je, nina mwelekeo wa kuisoma Biblia yote kwa jicho la kuelekea njia ambazo andiko hili au Maandiko haya yanaweza kuwa na muunganiko na maisha na ufunuo uliomo katika Agano la Kale, au na maisha na kazi ya Yesu wa Nazareti ambaye ni utimilifu wa Agano la Kale na ukamilifu wa ufunuo wa Agano Jipya? Kwa namna gani? • Je! ningeweza kuandika kile ambacho Agustino alisema: “Katika Agano la Kale Agano Jipya limefichwa; katika Agano Jipya Agano la Kale limefunuliwa.” Je, namna ninavyoshughulika na Maandiko inaonyesha ni kwa kiwango gani ninaamini katika umoja wa Agano la Kale na Agano Jipya? • Katika kanisa ninaloabudu, je, mahubiri na mafundisho yanaakisi uhusiano kati ya Agano la Kale na Agano Jipya ambao tumeuona kupitia mjadala wetu kuhusu mahusiano kamilishi kati ya maagano hayo (yaani, kwamba Agano la Kale linatoa utangulizi wa hitimisho la Agano Jipya kuhusu Kristo, Agano la Kale linamtarajia Masihi na kazi yake, huku Agano Jipya likimtambulisha Yesu wa Nazareti kama kilele cha matarajio hayo, nk.)? • Je, ninamwabudu na kumtumikia Mungu kwa kiasi gani nikiwa na aina hii ya ufahamu wa kihistoria ambao unatokana na dhana ya ahadi na utimilifu ? Je, nina kawaida ya kukazia fikira wakati uliopita, wa sasa, au wakati ujao katika usomaji wangu wa Biblia, kutafakari, na sala? • Je, mimi huelekea kumwona Yesu kuwa uzao wa mwanamke ambaye ataharibu kazi ya ibilisi, na vilevile mzao wa Abrahamu ambaye kupitia kwake familia zote za dunia zitabarikiwa? Je, ni njia gani ya msingi ninayomwona Yesu katika mwanga wa mafunuo haya kumhusu? • Je, mimi (mara nyingi) ninathibitisha mafundisho ya Yesu kwamba yeye mwenyewe ndiye mada kuu na ujumbe wa ufunuo wote wa Biblia (taz. Luka 22:25-27, 44-48; Mt. 5:17 18; Yoh. 1:45; 5:39-40 ; Ebr 10:5-10 ling. na Zab. 40:6-8)? Je, ninatumiaje Biblia mara nyingi maishani mwangu – kama uthibitisho wa nafsi ya Yesu au zaidi kuhusiana na shida zangu, mahitaji, na masuala yanayonikabili? Je, tunapaswa kutumiaje Agano la Kale kwa kuzingatia mafundisho ya Yesu kulihusu?

3

M A S O M O Y A B I B L I A

Made with FlippingBook Digital Proposal Maker